Habari za Punde

MAFINGA SENSABIKA FESTIVAL KUFANYIKA MJINI MAFINGA

Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini Mhe.Cosato Chumi akiwa na viongozi wa serikali ya wilaya na halmashauri ya Mafinga Mji wakati wakigawa vifaa vya michezo kwa ajili ya kesho kwenye Mafinga SENSABIKA festival litakalo fanyika katika mji wa mafinga.
Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akiwa na viongozi wa serikali ya wilaya na halmashauri ya Mafinga Mji wakati wakigawa vifaa vya michezo kwa ajili ya kesho kwenye Mafinga SENSABIKA festival litakalo fanyika katika mji wa mafinga. 

Na Fredy Mgunda, Iringa.

Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mji Cosato Chumi kwa ushirikiano,uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mufindi wameanda tamasha kubwa litakalo fanyika katika uwanja wa Wambi Mafinga Mjini kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhesabiwa siku ya tarehe 23 mwezi wa nane mwaka 2022 ili kuiwezesha serikali kujua takwimu za wananchi.

Akizungumza na blog hii mbunge wa Jimbo la Mafinga Mji Cosato Chumi alisema kuwa lengo la tamasha hili ni kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhesabiwa siku ya SENSA kwa ajili ya maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Chumi alisema kuwa wameamua kuiunga mkono juhudi za serikali katika kuhakikisha wananchi wote wanajitokeza kuhesabiwa siku ya SENSA tarehe 23/8/2022 kwa lengo kubwa la kuisaidia kupanga bajeti ya maendeleo kwa wananchi wa maeneo husika.

Alisema kuwa Mafinga SENSABIKA festival linatoa ujumbe kwa wananchi umuhimu wa SENSA ya watu na makazi kwa ajili ya maendeleo ya taifa la Tanzania.

Alisema kuwa serikali ikijua idadi maalamu ya wananchi wa maeneo husika itasaidia serikali kutatua changamoto na kupeleka kupeleka maendeleo kulingana na idadi ya wananchi wa maeneo husika.

Chumi alimazia kusema kuwa faida ya SENSA hii ndio dira ya miaka kumi ya Taifa la Tanzania hivyo wananchi wanapaswa kujitokeza kuhesabiwa siku ya SENSA.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mufindi Saad Mtambule alisema kuwa wameshakuwa wanatoa elimu mara kwa mara juu ya umuhimu wa kuhesabiwa siku ya tarehe 23/8/2022.

Mtambule alisema kuwa wananchi wa mji wa mafinga wanatakiwa kujitokeza kwa wingi siku ya kesho kwenye Bonanza la Mafinga SENSABIKA festival ambalo litafanyika katika uwanja wa Wambi Mafinga Mjini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.