Habari za Punde

Ufunguzi wa Mashindano makubwa ya kusoma na kuhifadhi Quran Tukufu Msitiki wa Kinondoni

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndg Abdulrahman Kinana na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Alhaj Dkt. Abubakar Zubeir bi Ali wakiongea na Katibu Mkuu wa Taasisi ya Mohamed VI Foundation Dkt. Sidi Mohamed Rifki mara baada ya ufunguzi wa Mashindano makubwa ya kusoma na kuhifadhi Quran Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Mfalme Mohamed VI  (Mohamed VI Foundation) katika Masikiti Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Kinondoni Muslim jijini Dar es salaam leo Ijumaa Agosti 12, 2022.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndg Abdulrahman Kinana na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Alhaj Dkt. Abubakar Zubeir bi Ali, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Jumanne Muliro (kushoto) na viongozi wengine katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Taasisi ya Mohamed VI Foundation Dkt. Sidi Mohamed Rifki mara baada ya ufunguzi wa Mashindano makubwa ya kusoma na kuhifadhi Quran Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Mfalme Mohamed VI  (Mohamed VI Foundation) katika Masikiti Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Kinondoni Muslim jijini Dar es salaam leo Ijumaa Agosti 12, 2022.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi akiwa katika picha ya kumbukumbu na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Alhaj Dkt. Abubakar Zubeir bi Ali,  Katibu Mkuu wa Taasisi ya Mohamed VI Foundation Dkt. Sidi Mohamed Rifki (wa tatu toka kulia) pamoja na viongozi wengine mara baada ya ufunguzi wa Mashindano makubwa ya kusoma na kuhifadhi Quran Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Mfalme Mohamed VI  (Mohamed VI Foundation) katika Masikiti Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Kinondoni Muslim jijini Dar es salaam leo Ijumaa Agosti 12, 2022.

Picha na Issa Michuzi

Na Issa Michuzi, Kinondoni
Mashindano makubwa ya kusoma na kuhifadhi Quran Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Mfalme Mohamed VI  (Mohamed VI Foundation) wa Morocco yamefunguliwa rasmi leo katika Masikiti Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Kinondoni Muslim jijini Dar es salaam huku nchi 35 zikishiriki.

Pamoja na mashindano hayo, ambayo ni katika awamu yake ya tatu yakiwa yameanzia nchini Morocco na kisha Senegal, pia kuna maonesho maalum ya Quran ikiwa ni pamoja na jinsi kitabu hicho Kitukufu kwa Waislamu duniani kinavyoandikwa kwa mkono na kwa mashine.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi alihudhuria ufunguzi huo ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndg Abdulrahman Kinana, aliyewaongoza maelfu ya waumini katika hafla hiyo iliyoambatana na Swala ya Ijumaa.

Ndg Kinana amemshukuru Mfalme wa Morocco sio tu kwa kuichagua Tanzania kuwa nchi ya tatu kuandaa mashindano hayo makubwa bali pia kwa kujenga msikiti huo mkubwa kuliko yote katika nchi za Afrika Mashariki na kati, kufuatia ziara yake nchini mnamo Oktoba 2016.

"Ziara hiyo ya Mfalme Mohamed VI nchini imeendeleza uhusiano mwema uliopo kati ya nchi hizi mbili pamoja na kufungua milango ya nyanja mbalimbali ikiwemo dini na bishara", amesema Ndg. Kinana.

Katibu Mkuu wa Taasisi ya Mohamed VI Foundation Dkt Sidi Mohamed Rifki ameusifia uongozi wa tawi la Taasisi hiyo nchini chini ya Mwenyekiti wake Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Alhaj Dkt. Abubakar Zubeir bi Ali, kwa weledi mkubwa uliotumika katika kuandaa mashindano hayo.

Dkt. Rifki amelihakikishia Tawi la Taasisi hiyo nchini utekelezaji wa programu zake kwa mujibu wa maazimio iliyoijiwekea ya kuendeleza dini na vijana, pamoja na kuendeleza umoja wa wana Ulamaa katika kuhakikisha usalama, Uimara na maendeleo ya bara la Afrika.

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Alhaj Dkt. Abubakar Zubeir bi Ali amewataka Watanzania bila kujali itikadi ya dini kuhudhuria mashindano hayo ambayo yanafikia tamati siku ya Jumapili.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.