Habari za Punde

 

Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Mhe.Rajab Mkasaba akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi wa michezo mbalimbali iliyofanyika wakati wa Tamasha la Kizimkazi lililofikia kilele chake Septemba 3 , katika viwanja vya Kizimkazi Dimbani Mkoa wa Kusini Wilaya Kusini Unguja.
Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Mhe.Rajab Mkasaba akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi wa michezo mbalimbali iliyofanyika wakati wa Tamasha la Kizimkazi lililofikia kilele chake Septemba 3 , katika viwanja vya Kizimkazi Dimbani Mkoa wa Kusini Wilaya Kusini Unguja.
Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Mhe.Rajab Mkasaba akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi wa michezo mbalimbali iliyofanyika wakati wa Tamasha la Kizimkazi lililofikia kilele chake Septemba 3 , katika viwanja vya Kizimkazi Dimbani Mkoa wa Kusini Wilaya Kusini Unguja.

WASHINDI wa michezo mbali mbali ya Tamasha la Kizimkazi wamepomgezwa kwa ushiriki wao hatua ambayo imeonesha jinsi wanavyoendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ndio muasisi na mlezi wa Tamasha hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Kusini Rajab Yussuf Mkasaba ameyasema hayo mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi mbali mbali wa michezo iliyofanyika katika Tamasha la Kizimkazi hivi karibuni, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Sheha wa Shehia ya Kizimkazi Dimbani.

Katika maelezo yake Mkuu huyo wa Wilaya aliwapongeza wanamichezo hao kwa ushiriki wao huo na kuwasisitiza kuendelea kushiriki katika michezo hiyo hapo mwakani kwa azma ya kuendelea kumuunga mkono muasisi na mlezi wa Tamasdha hilo Rais Samia Suluhu Hassan.

Alisema kuwa kuwepo kwa michezo hiyo kumeongeza ladha ya Tamasha hilo kwani wanamichezo na wananchi wa Wilaya hiyo wameweza kushiriki vyema pamoja na kuendelea kujenga umoja, mshikamano na udugu walio nao kupitia mashindano hayo.

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya alieleza umuhimu wa michezo huku akiwataka washindi kuendelea kushika nafasi zao na wale walioshindwa kujitahidi hapo mwakani ili na wao wawe washindi na hatimae wapate zawadi nono.

Pamoja na hayo Mkasaba alitumia fursa hiyo kuwapongeza wanamichezo wote walioshiriki katika michezo ya Tamasha hilo ambacho kilele chake kilifanyika Septemba 3, mwaka huu huko Kizimkazi Dimbani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan alikuwa ndie mgeni rasmi.

Mkasaba pia, alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kulilea tamasha hilo pamoja na kuungana na wananchi wa Wilaya hiyo kwa kuwazindulia miradi yao sita ya maendeleo kwa siku moja mnamo Septemba 2, 2022 siku moja kabla ya kilele cha Tamasha hilo.

Pia, alitumia fursa hiyo kuipongeza benki ya CRDB kwa kudhamini mashindano hayo pamoja na kuipongeza Kamati ya Tamasha la Kizimkazi kwa kuratibu vyema shughuli hizo huku akiwapongeza viongozi na wananchi waliohudhuria katika Tamasha hilo linalofanyika kila mwaka katika Wilaya hiyo.

Miongoni mwa michezo iliyoshindaniwa katika Tamasha hilo la Kizimkazi ni mpira wa miguu, mpira wa pete, nage, ngalawa, kuvuta kamba, baskeli, bao la kete, karata, chanis, karata wahedi wa60, drafti, kufua na kukuna nazi, kusokota kamba pamoja na mashindano ya michezo mitano kwa wanafunzi wa skuli za maandalizi.

Sambamba na hayo pia, Mkuu wa Wilaya hiyo alitoa zawadi kwa washindi wa  mashindano ya “General knowledge kidato cha Pili” ambayo yaliwashirikisha wanafunzi kutoka skuli ya Sekondari Hasnu Makame, Skuli ya Sekondari Kizimkazi Dimbani na Skuli ya Sekondari Kizimkazi Mkunguni. Pia alitoa zawadi kwa washindi wa mashindano ya kuhifadhi Quran.

Mashindano yote hayo yaliwashirikisha wanaume na wanawake ambazo zawadi za fedha taslim zilitolewa kwa washindi pamoja na washiriki wote ambapo kiasi cha TZS milioni 26,780,000 zilitolewa.

Imetayarishwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kusini,

Mkoa wa Kusini Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.