.JPG)
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akifungua warsha ya siku mbili ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya buluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary
Masanja amefungua warsha ya siku mbili ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia
wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa
ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya
misitu nchini.
Warsha hiyo imefunguliwa Septemba 27,2022
katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika ufunguzi huo, Mhe. Masanja amesema
misitu ya mikoko na majani ya baharini inatarajiwa kuchangia katika ukuaji wa
uchumi wa bluu kwa kuhifadhi hewa ya ukaa mara tano zaidi ya misitu ya kawaida.
Ameelekeza washiriki wa warsha hiyo kuibua masuala
muhimu yatakayoisaidia Serikali kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya biashara
ya hewa ya ukaa.
Ametaja faida nyingine za misitu ya mikoko kuwa
ni kusaidia kukabiliana na athari za kimazingira kama mabadiliko ya tabia ya
nchi, mmomonyoko wa udongo na vimbunga baharini, kusaidia uwepo wa mazalia ya
samaki, chanzo cha kuni, mbao na milunda ya kujengea.
Aidha, amesema uwepo wa shughuli za kibinadamu
katika misitu ya mikoko, hupelekea kupotea kwa mikoko na kuathiri ukuaji wa
uchumi wa bluu.
Mhe. Masanja amefafanua kuwa ili kukabiliana na
changamoto za upotevu wa misitu ya mikoko Serikali itatoa elimu kwa wananchi
namna bora ya kutunza mikoko hiyo na kushiriki moja kwa moja katika uhifadhi wa
mikoko kwa kushirikiana na sekta binafsi.
Naye, Kamishna wa Uhifadhi, Wakala wa Huduma za
Misitu za Misitu Tanzania, Prof Dos Santos Silayo amesema wananchi wanatakiwa
wawe na mifumo endelevu ya kupata kipato itakayowawezesha kukidhi mahitaji yao bila
kukata mikoko.
“Mifumo hii itawawezesha wananchi kuvuna hewa
ya ukaa na kujipatia fedha bila kuathiri mikoko kwa mfano kufanya shughuli za
ufugaji nyuki na utalii” amefafanua
Prof. Silayo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uvuvi, Wizara ya
Uchumi wa Buluu Zanzibar, Dkt. Salumu Hemedi amesema kuna uhusiano mkubwa wa
uchumi wa bluu na biashara ya hewa ya ukaa.
Amesema biashara ya hewa ya ukaa inafanyika
sana katika mataifa mengi duniani ambayo yana viwanda yanatumia hewa ya ukaa
katika nchi ambazo zina misitu ambazo zinalipwa ili kutunza misitu.
Warsha hiyo imehudhuriwa wa Maafisa kutoka
Serikali ya Tanzania na Kenya, Wawakilishi wa Sekta Binafsi, Wadau wa
Uhifadhiwa Mifumo Ikolojia ya Buluu pamoja na Balozi wa Uholanzi nchini
Tanzania..JPG)
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (kulia) na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe. Jeroen Verheul (kushoto) wakikata utepe kama ishara ya kufungua warsha ya siku mbili ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe. Jeroen Verheul akizungumza katika warsha ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki, Wizara ya Maliasili na Utalii,Deusdedit Bwoyo akitoa maneno ya utangulizi katika warsha ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Uhifadhi, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo akizungumzia namna taasisi yake inavyoshiriki katika utunzaji wa misitu ya mikoko katika warsha ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (hayupo pichani) akifungua warsha ya siku mbili ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (katikati)katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya wadau wa uhifadhi mfumo wa ikolojia wa hewa ya ukaa ya bluu na uendelezaji wa uchumi wa bluu Tanzania, lengo ikiwa ni kujadili namna bora ya kuondokana na changamoto zinazoikabili sekta ya misitu nchini iliyofanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment