Habari za Punde

Rais Mhe Samia Suluhu Hassan Atimiza Ahadi ya Shilingi Milioni 50 kwa Ujenzi wa Kanisa la KKT Ikulu Chamwino Dodoma

 

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akipokea barua maalum ya kumpongeza Rais kutoka kwa Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)Dayosisi ya Dodoma Amoni Kinyunyu.

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.                                                   

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan ametimiza ahadi ya Tsh.Milioni 50  aliyoahidi hivi karibuni kwa ajili ya ujenzi wa kanisa la Kiinjili Kilutheri Tanzania(KKKT) Usharika wa  Chamwino Ikulu.

 Akizungumza Leo Septemba 18,2022  kwa niaba ya Rais katika kanisa hilo mara baada ya kukabidhi  hati ya cheti cha udhibitisho wa pesa hiyo iliyotolewa katika benki ya NMB mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewataka watanzania husan Mkoa wa Dodoma kutumia fursa zilizopo ikiwemo mradi wa treni ya umeme kipande cha Morogoro hadi Makutupora ambao umefikia asilimia 89%.

"Rais Samia amenituma nije nikabidhi hati hii kuwa Tsh.Milioni 50 tayari zimeshawekwa kupitia akaunti ya 52810010215 NMB yenye jina KKKT UJENZI IKULU CHAMWINO,Rais Samia ametoa hizo fedha kwani ana hofu ya Mungu nawasihii tuchangamkie fursa zinazotuzunga"amesema.

Hivyo amesisitiza kuwa ni lazima kijitafakari kila mwanadodoma ananufaikaje na fursa za Dodoma .

"SGR imeajiri watu 6000,ofisi za Dodoma zipo wazi zitumieni fursa hizo

 Aidha,Senyamule  amesema kati ya viongozi wanaotaka watanzania waishi kwa haki bila kuonewa ni Rais Samia hivyo na kuwasihi waumini waendelee kumwombea kwa Mungu jambo alilofanya .

 Pia,mkuu huyo wa Mkoa amebainisha mikakati kabambe wilayani Chamwino kuwa ni pamoja na miradi ya kilimo maeneo ya kimkakati mawili moja likiwa na hekta 8000 na linalofuatia likiwa na hekta 11000

.Kwa upande wake Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)Dayosisi ya Dodoma Amoni Kinyunyu ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuchangia milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa la KKKT Chamwino Ikulu .

Hivyo,kanisa limemwandikia Rais Samia  barua maalum ya kumpongeza huku KKKT Dayosisi ya Dodoma ikitoa mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kanisa.

"Mungu ambariki sana Rais wa Tanzania anazungumza kwa vitendo sio kwa maneno,tunaona mwendelezo wa kuhamia Dodoma,miradi mikubwa kuendelea kujengwa ni kwa vitendo"amesema.

 Pia,amesema kutokana na fedha walizopata kutoka kwa Rais Samia haitawafanya wabweteke na wataendelea kuongeza msukumo wa michango .

 Aidha,amezungumzia umuhimu wa kuweka akiba na tumaini kwa Yesu Kristo .

"Unakuta watu wengine wanaweka matumaini  na wanafanya maombi makaburini ili wabarikiwe,makaburi hayatoi baraka,jiwekee hazina mbingu kwa kuweka tumaini kwa Mungu"amesema.

 Amesema mahala pekee penye mibaraka ni kwa Mungu hivyo wakristo wanatakiwa kujiwekea akiba kwake kwani ni hazina kuu.

 Askofu Kinyunyu amesema watumishi wa serikali na sekta binafsi nao pia wanatakiwa kujiwekea akiba ili kuondokana na changamoto za kiuchumi pindi wanapostaafu.

"Anza kuweka akiba ukijua kuwa miaka 7 za neema na miaka 7 za njaa ,usharika anza kuwa na mfuko wa akiba matumbo hizi fedha hazitoshi"amesisitiza.

 Hata hivyo,Askofu Kinyunyu amesema  Sasa kanisa limejikita katika uinjilisti wa kutopiga makelele .

"Uinjilisti tunaotaka kujikita zaidi ni wa vitendo na si kupiga kelele "amesisitiza.Awali akitoa taarifa fupi ya ujenzi wa kanisa la KKT usharika wa Chamwino Ikulu   Afisa miradi  Dickson Mlela amesema gharama za jengo la kanisa hilo ni Tsh.Milioni mia tatu ishirini na sita,laki sita sabini na saba elfu na mia Tano( 326,677,500).

 Ikumbukwe kuwa  Katika ibaada ya harambee ya tarehe 28/08/2022 ,mifuko ya saruji 236,fedha taslimu Tsh.10,132,000 na ahadi Tsh.17,407,000 ikiwa ni jumla ya Tsh.27,539,000 zilipatikana huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akichangia taslimu Tsh.Milioni 50.

Hata hivyo,bado kuna upungufu wa fedha kiasi cha Tsh.milioni 144,285,290  kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kanisa.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary  Senyamule kwa niaba ya Rais Samia  akikabidhi hati ya cheti cha udhibitisho wa fedha Tsh.Milioni 50  kwa  mchungaji kiongozi  KKKT  ushirika wa Chamwino Ikulu      Mch. Anold Chambulila .
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akihutubia katika ibaada iliyokwenda sambamba na utoaji wa hati ya cheti cha Tsh.milioni 50 ahadi ya Rais Samia  katika kanisa la KKT kwa ajili Ujenzi usharika wa Chamwino Ikulu.
Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)Dayosisi ya Dodoma Amoni Kinyunyu

Mkuu wa wilaya ya Chamwino  Gift Msuya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.