Habari za Punde

Taasisi ya NDI Yapongezwa kwa Kazi Nzuri Inayofanya kwac Kushirikiana na Asasi za Kiraia Nchini.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Taasisi ya Kidemokrasia Inayoshughulikia Masuala ya Kimataifa (NDI) ukiongozwa na Mkurugenzi Mkazi Nchini Tanzania Bi. Sandy Quimbaya (kulia kwa Rais) ulipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika leo 1-9-2022 katika ukumbi wa Ikulu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi amekutana na Uongozi wa Taasisi  ya Kidemokrasia inayoshughulikia masuala ya Kimataifa (NDI), ukiongozwa na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo nchini Sandy Quimbaya, ambapo  ulifika Ikulu kujitambulisha na kuelezea shughuli inazofanya.

Akizungumza na ujumbe huo pamoja na mambo mengine  Dk. Mwinyi aliipongeza taasisi hiyo kwa kazi nzuri inayofanya kwa kushirikiana na  Asasi za kiraia hapa nchini.

Akigusia dhana ya  NDI  juu ya uwepo wa Serikali  ya Umoja wa Kitaifa (GNU) , Dk. Mwinyi alisema ni eneo muhimu kwa msingi kuwa  Serikali hiyo unaimarisha umoja wa Taifa na wananchi wake, pamoja na kudumisha amani, ikiwa ni hatua muhimu kufikia maendeleo ya kiuchumi.

Alisema kupitia Asasi za Kiraia NDI imefanya  kazi nzuri ya kuwafikia wananchi na hatimae kupendekeza nini kifanyike ili kuwa na  Serikali y yenye mfumo wa  Umoja wa Kitaifa ilio imara zaidi.

Alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suliuhu Hassan kwa kuanzisha ‘Kikosi kazi’, huku akibinisha umuhimu wa kuwa na ‘kikosi kazi kidogo’  kitakachokuwa maalum kwa ajili ya kushughulikia changamoto zinazoikabili Zanzibar pekee.

Aidha, Dk. Mwinyi aliunga mkono hatua ya NDI inayolenga kusaidia kuwainua kiuchumi wananchi, ikiwemo wakulima wa zao la mwani.

Nae, Mtafiti kutoka Asasi za Kiraia ya JUWAUZA Rashid Azizi, akichambua dhana ya Mradi wa Serikali ya umoja wa Kitaifa (GNU) na changamoto zilizopo, alisema utafiti umebainisha wananchi walio wengi nchini wanaunga mkono uwepo wa GNU.

Alisema, kwa mujibu w aamelezo ya wananchi uwepo wake umesaidia sana kuimarisha hali ya amani na umoja mongoni mwa Wazanzibari, huku wakipongeza hatua ya Rais Dk. Mwinyi ya kuweka  utaratibu wa kutembelea nyumba za Ibada (misikiti) na kuhubiri umoja.

Azizi alibainisha baadhi ya mambo ambayo wananchi wanahisi kuwa ni changamoto  katika GNU, ikiwemo upatikanaji wa Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi, kwa kigezo kuwa wanachelewa kuvipata pamoja na kutolewa kwa misingi ya itikadi  za kisiasa.

Alisema mchakato wa uchaguzi ni eneo jengine ambalo wn anachi wanaelezea kuwa lina changamoto na kubainisha umuhimu wa  kuwepo uwazi tangu hatua za awali za uandikishaji.

Aidha, alisema wananchi walio wengi hususan wale walioko Vijijini wamaelezea umuhimu wa kupatiwa huduma mbali mbali muhimu za kijamii.

Alisema upatikanaji wa ajira ni eneo ambalo wananchi wanalalamikia na  kuishauri Serikali haja ya  kuwepo mfumo unaozingatia weledi  huku akisisitiza umuhimu wa kuongeza nguvu katika usimamizi, kupitia mfumo wa Mtandao wa  ZAN Ajira.

Kuhusiana na Uchumi wa Buluu, Mchambuzi huyo alisema wananachi wamependekeza kuongezewa thamani zao la Mwani kwani bei inayolipwa hivi sasa na Kampuni zinayojishughulisha na ununuzi wa zao hilo ni ndogo mno, huku wakilalamika kuwa baadhi ya wanunuzi hao kuwa hawaaminiki.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Taasisi ya Kidemokrasia Inayoshughulikia Masuala ya Kimataifa (NDI) ukiongozwa na Mkurugenzi Mkazi Nchini Tanzania Bi. Sandy Quimbaya (kulia kwa Rais) ulipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika leo 1-9-2022 katika ukumbi wa Ikulu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Ripoti ya Sisi ni Wamoja, Mtazamo wa Wananchi Kuhusu Serikali ya Umoja wa Kitaifa, utafiti uliofanywa na Jumuiya ya Wanawake Wenye Ulemavu Zanzibar, akikabidhiwa na Ndg.Rashid Azizi Rashid (kulia kwake) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA) Bi. Salma Haji Saadat, baada ya kumaliza mazungumzo na Uongozi wa Taasisi ya Kidemokrasia Inayoshughulikia Masuala ya Kimataifa (NDI) yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 1-9-2022
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Kidemokrasia Inayoshughulikia Masuala ya Kimataifa (NDI) Bi. Sandy Quimbaya, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 1-9-2022

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.