Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Amuwakilisha Rais Mhe Samia Nchini Japan

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo (Jumamosi, Septemba 24, 2022) kwenda Tokyo, Japan ambako atamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mazishi ya  kitaifa ya Waziri Mkuu mstaafu nchi hiyo, Bw. Shinzo Abe. Pichani  Waziri Mkuu,  akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Uhirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk kabla ya kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Mkoani Dar es salaam. Kushoto ni mkewe mary na wapili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo (Jumamosi, Septemba 24, 2022) kwenda Tokyo, Japan ambako atamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mazishi  ya kitaifa ya Waziri Mkuu mstaafu nchi hiyo, Bw. Shinzo Abe. Pichani  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Uhirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk kabla ya kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Mkoani Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo (Jumamosi, Septemba 24, 2022) kwenda Tokyo, Japan ambako atamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mazishi ya ya kitaifa ya Waziri Mkuu mstaafu nchi hiyo, Bw. Shinzo Abe.

Taratibu za kutoa heshimaza mwisho zinatarajiwa kufanyika Jumanne, Septemba 27, mwaka huu kwenye ukumbi wa Nippon Budokan. Waziri Mkuu huyo mstaafu aliuawa Julai 8, mwaka huu kwa kupigwa risasi akiwa kwenye mkutano wa kampeni za kisiasa katika jiji la Nara nchini humo.

 

Bw. Abe ambaye anatajwa kuwa kiongozi aliyeshika wadhifa wa Waziri Mkuu wa Japan kwa muda mrefu katika historia ya Japan, aliingia madarakani kuanzia mwaka 2006 hadi 2007 na akarudi tena mwaka 2012 hadi 2020.

 

Akiwa Japan, Mheshimiwa Majaliwa atakutana na Waziri Mkuu wa Japan, Mheshimiwa Fumio Kishida.

 

(mwisho)

 

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 980,

40480 – DODOMA

JUMAMOSI, SEPTEMBA 24, 2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.