Habari za Punde

Airtel Afrika yatangaza kudhamini tamasha la mashindano ya wasanii la ‘The Voice Africa’

Mkurugenzi Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano (kushoto) pamoja na Meneja Uhusiano Jackson Mmando (kati kati) na Meneja Masoko Arnold Madale (kulia) wakionyesha bango baada ya kuzindua tamasha la muziki la The Voice AfrikaAirtel Afrika, Kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma bora za mawasiliano pamoja na  huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi leo imetangaza kudhamini tamasha la muziki la The Voice Afrika ambalo litanfanyika kwenye nchi 14 barani Afrika ambapo Airtel inafanya biashara.
Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmando (kushoto) akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza kuanza kwa shindano la muziki la The Voice AfrikaAirtel Afrika, Kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma bora za mawasiliano pamoja na  huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi leo imetangaza kudhamini tamasha la muziki la The Voice Afrika ambalo litanfanyika kwenye nchi 14 barani Afrika ambapo Airtel inafanya biashara.

Airtel Afrika, Kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma bora za mawasiliano pamoja na  huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi  kwenye nchi 14 Barani Africa, leo imetangaza kudhamini tamasha kabambe la mashindano ya wasanii na wanamuziki linalojulikana kama  The Voice Afrika na kulizindua rasmi jijini Lagos, Nigeria leo hii.

Tamasha la The Voice Africa ni shindano la muziki na burudani  namba moja duniani linalooneshwa kwenye runinga ndani ya nchi zaidi ya 180. Tamasha hili limejizolea umaarufu na kuwa na mafanikio makubwa kupitia The Voice Nigeria., kupitia mafanikio hayo Airtel Afrika imeungana na waandaji wa msimu wa tatu na wanne, FAME Studios Afrika, kufanikisha tamasha hilo litakalowazawadia pia washiriki katika nchi 14 ambazo Airtel Afrika inafanya biashara.

Msimu huu wa The Voice Afrika utaonyesha moja kwa moja kwa mamilioni ya Waafrika  kupitia Airtel TV, vituo vya kurusha matangazo bure pamoja na chaneli za kulipia kwa nchi 14 Barani Afrika. Tamasha hili linategemewa kuwa kivutio kwani litavumbua na kuonesha vipaji vingi vya Waafrika kwenye muziki, Vilevile watakuwepo wataalam wa Sanaa, waalimu wabobezi na waandaji wa vipindi vya TV ambao watawezesha vijana wetu kuonekana kimataifa. Washiriki saba kutoka katika kila nchi 14 watachanguliwa kulingana na uwezo wao na hatimaye mmoja wao kutawazwa kuwa Bingwa wa The Voice Afrika.

Mkurugenzi Mtendaji Airtel Afrika Segun Ogunsanya alisema, “Kama wafanya biashara tunaendeshwa na dhamira ya kuwezesha na kubadilisha maisha ya watu wetu, na hii inakamilika kwa kufungua fursa mbalimbali ili waweze kukua. The Voice Afrika inatupa jukwaa la kusaidia kugundua vipaji vya muziki kwa vijana wa Kiafrika na kuweza kuwawezesha kufikia malengo yao. Naamini kuwa tamasha hili litaleta burudani yenye msisimko mkubwa na kuunganisha wanafamilia na wateja wetu wote barani Afrika”.

Mkurugenzi Mtendaji FAME Studios Akin Salami na Mtayarishaji Mtendaji The Voice Afrika alisema, “Tunayo furaha kwa kuanzisha tamasha la The Voice Afrika msimu wa kwanza na hasa kwa wakati kama huu ambao kuna ongezeko la krukubalika kwa muziki wa Afrika duniani. Mpango huu umetokana na shauku ya kuonyesha vipaji vya Kiafrika kwenye jukwaa la kimataifa na kujenga mustakabali wa Afrika kutambukika zaidi kupitia burudani. Tunatarajia kuwa msimu huu wa kwanza utakuwa wa kusisimua na wenye burudani ya aina yake – msimu ambao utawaacha mashabiki na wapenzi wa kipindi hiki wakitamani Zaidi”.

Akiongea na waandishi wa Habari pamoja na baadhi ya wanamuziki katika mkutano maalum wa kutambulisha tamasha hilo nchini Tanzania Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Bi Beatrice Singano alisema “Watanzania naomba tuchangamkie fursa hii ili kuitangaza nchi yetu kupitia burudani, Muziki wetu sasa unamchango mkubwa katika kujitambulisha na kuitangaza  nchi katika anga za kimataifa, Sasa uwepo wa Tamasha hili la The Voice of Afrika ni jukwaa jingine la kuipaisha burudani yetu Pamoja na kuitangaza nchi yetu ili kuunga mkono jitiada za Raisi wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan wetu kuitangaza nchi Kupitia Sanaa kama alivyofanya yeye Kupitia Royal Tour”.

Singano alitaja nchi zingine zitakazoshiriki kuwa ni nchi yetu TanzaniaNigeria, Niger, Zambia, Kenya, Malawi, Madagascar, Seychelles, Rep of Congo, Chad, Rwanda, DRC, Gabon and Uganda

Ushirikiano wa ubunifu wa Airtel Afrika na The Voice utaleta msisimko kwa mashabiki kupitia muunganisho wa maudhui maalum hewani, uanzishaji wa mitandao ya kijamii na kidigitali na matukio ya kila nchi. The Voice Afrika itaanza na mwito wa kujiandikisha kwa njia ya mtandaoni tarehe 19 Oktoba na kufuatiwa na majaribio kutumbuiza moja kwa moja baadaye mwaka huu. Kipindi hiki kitatangazwa Machi 2023 na fainali itafanyika baadaye mwakani. Kwa maelezo Zaidi, tafadhali tembelea www.thevoice.afrika.com.

Kuhusu Kujiandisha ili kushiriki The Voice Afrika

          .   Kujiorodhesha/kujiandikisha ni BURE kupitia www.thevoice.africa.com

  • Mshiriki lazima awe na umri wa miaka 18 na Zaidi, awe na kitambulisho kinachotambulika serekalini ikiwemo hati ya kusafiria

  • Awe na namba ya iliyosajiliwa kiukamilifu ya Airtel atakayotumia kujiandikisha kushiriki The Voice Afrika.
  • Mwisho wa kutuma video fupi kwaajili ya kufanyiwa usahili ni Jumapili Novemba 6, 2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.