Mshambuliaji wa Timu ya Chipukizi akijaribu kumpita beki wa Timu ya Mafunzo wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya PBZ Zanzibar mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Unguja Jijini Zanzibar.Timu ya Chipukizi imeshinda mchezo huo kwa bao.1-0.
TIMU za soka za Chipukizi na Jamhuri zimeibuka na ushindi Katika michezo yao ya Ligi kuu ya Zanzibar waliyocheza kwenye viwanja tofauti.
Chipukizi iliyoshuka uwanja wa Amaan iliifunga mabao 2-1, wakati Jamhuri iliifunga Mlandege bao 1-0 katika mchezo uliochezwa uwanja wa Finya Kisiwani Pemba.
Chipukizi katika mchezo huo mabao yake yalifungwa na Faki Mwalimu Sharif dakika ya 29 na Mafunzo bao lao lilifungwa na Jaku Joma dakika ya 52.
Katika mchezo huo Mafunzo ilicheza wakiwa pungufu baada ya mchezaji wao Muhammad Omary Abdalla kutolewa nje na mwamuzi Mfaume Ali kwa kumfanyia faulu Philemon Abdul Mselem.
Kwa upande wa timu ya Jamhuri ambayo ushindi huo imefikisha pointi nane na kupanda nafasi moja juu kutoka wa 10 hadi wa 11 bao lake la pekee lilifungwa na Abdulkarim Khamis Faki.
Kwa matokeo ya mchezo huo Chipukizi imefikisha pointi 14 na kuwa nafasi ya pili ya msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na Malindi wenye pointi sawa ila ipo juu kwa magoli ya kushinda na kufungwa.
No comments:
Post a Comment