Habari za Punde

Mama Mariam Mwinyi afanya mazungumzo na Makamo wa Rais wa Taasisi ya Rockfeller

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi pia Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation ZMBF (katikati) leo amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Taasisi ya Rocke Feller Bw,Andrew Sweet(wa tatu kushoto) katika kuiwesha na kusaidia mfumo wa kutoa Chanjo ya Covid -19 kwa Wilaya ya Magharibi "A" na Kaskazini "A" Unguja . [Picha na Ikulu] 25/10/2022.


Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi pia Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation ZMBF (kulia) akizungumza na Ujumbe wa Taasisi ya Rocke Feller unaoongozwa na Makamo wa Rais wa Taasisi hiyo Bw,Andrew Sweet(wa pili kulia) katika kusaidia na kuwezesha mfumo wa kutoa Chanjo ya Covid -19 kwa Wilaya ya Magharibi "A" na Kaskazini "A" Unguja,mazungumzo hayo yalifanyika leo katika Ofisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation ZMBF Migombani. [Picha na Ikulu] 25/10/2022.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi pia Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation ZMBF (kushoto) abadilishana mawazo na Makamo wa Rais wa Taasisi ya Rocke Feller Bw,Andrew Sweet mara baada ya  leo mazungumzo yaliyofanyika leo katika Ofisi ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation ZMBF iliyopo Migombani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,mazungumzo hayo yaliyoashiria katika kuiwezesha na kusaidia mfumo wa kutoa Chanjo ya Covid -19 kwa Wilaya ya Magharibi "A" na Kaskazini "A" Unguja . [Picha na Ikulu] 25/10/2022

MKE  wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mariamu Mwinyi ameishukuru Jumuiya Health Rockfeller Foundation  kutoka nchini Marekani kwa azma  yake za kusaidia juhudi za Serikali katika kujikinga na Ugonjwa wa Covid -19.

 

Mama Mariamu ambae pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) ametoa shukurani hizo Ikulu  Migombani mara baada ya mazungumzo na Ujumbe wa Jumuiya Health Rockfeller Foundation ulioongozwa na Makamo wa Rais Andrew Sweet, ambapo Jumuiya hiyo itasaidia Progamu ya utoaji wa chanjo za Ugonjwa wa Covid-19 hapa nchini.

 

Amesema  ZMBF inathamin juhudi za Jumuiya hiyo kwa vile inayolenga kuimarisha afya za wananchi katika kujikinga na ugonjwa huo.

 

Alisema mradi huo ni wa mwaka mmoja itatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Jumuiya hizo mbili , AMREF pamoja na Wizara ya Afya katika Wilaya za Magharibi ‘A’ pamoja   Kaskazini ‘A’ Unguja .

 

Nae, Makamo wa Rais wa  Jumuiya ya Health Rockfeller Foundation Andrew Sweet alisema ni jambo la faraja kwa Jumuiya hiyo kuwa na ushirikiano na ZMBF na kupata fursa ya kuwasaidia huduma za chanjo ili wananchi waweze  kukabiliana na ugonjwa Covid -19

 

Aidha, Mjumbe wa Bodi ya ZMBF Dk. Ellen Mkondya Senkoro alisema Programu inayolengwa kutekelezwa ni kubwa  na kubainisha matumaini yake kuwa mradi huo utatowa matokeo chanya.

 

Imetayarishwa na Idaya ya Mawasiliano

Ikulu Zanzibar.

 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.