Habari za Punde

Serengeti Girls Waendelea Kujifua Kuikabili Ufaransa

 

Na Shamimu Nyaki

Timu ya Taifa ya Wasichana chini ya miaka 17 (Serengeti Girls) imeendelea na mazoezi   Oktoba 13, 2022 Uwanja wa Utorda Goa India.

Serengeti Girls ilianza na mazoezi ya asubuhi katika fukwe zilizopo eneo la Utorda na baadae katika uwanja wa eneo hilo.

Mazoezi hayo ni katika maandalizi ya Mechi dhidi ya Ufaransa itakayochezwa Oktoba 15 majira ya Saa 4:30 jioni saa za nchini India Uwanja wa Pandit Jawaharlal Nehru jijini Goa India. 

Katika mazoezi hayo Kaimu Mkurugenzi Idara ya Michezo Bw. Ally Mayay ameendelea kuwapa hamasa wachezaji hao kuwa uwezo wanao wakupambana  na  kuwakilisha vyema Taifa. Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Umri chini ya Miaka 17 (Serengeti Girls) inaendelea na mazoezi ya Mashindano ya Kombe la Dunia yanayoendelea  nchini India.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.