Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akikabidhiwa Taarifa fupi ya Usafishaji wa Mto Msimbazi kutoka kwa Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha kuratibu usafishaji wa Mito na Mabonde Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Elizabeth Mshote alipowasilisha ofisini kwa Waziri jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akipitia Taarifa fupi ya Usafishaji wa Mto Msimbazi mara baada ya kuipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha kuratibu usafishaji wa Mito na Mabonde Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Elizabeth Mshote na Kikosi chake walipowasilisha ofisini kwa Waziri jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo (katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na Kikosi kazi kilichowasilisha Taarifa ya fupi ya Usafishaji
wa Mto Msimbazi ofisini kwake jijini
Dodoma.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amepokea Taarifa fupi ya
usafishaji wa Mto Msimbazi kutokana na maelekezo aliyotoa hivi karibuni kwa
Kikosi cha kuratibu usafishaji Mito na Mabonde Mkoa wa Dar es Salaam.
Taarifa hiyo
imewasilishwa kwa Waziri Jafo ofisini kwake jijini Dodoma na Mwenyekiti wa
Kikosi kazi cha kuratibu usafishaji wa Mito na Mabonde Mkoa wa Dar es Salaam
Dkt. Elizabeth Mshote.
Hivi karibuni alifanya
ziara ya kikazi ya kukagua mto huo katika Kata ya Mogo Mtaa wa
Kipawa baada ya kupokea malalamiko kuhusiana na athari za kimazingira
zinazotokana na usafishaji wa mto huo.
Hata hivyo, wakati wa ziara hiyo
baada ya kusikiliza maoni ya wananchi alipata maoni yanayokinzana ambapo
wengine walidai shughuli za usafishaji mto huo zimeleta athari kwa mazingira na
wengine wakidai zimeleta manufaa makubwa kwa jamii inayozunguka eneo hilo.
Itakumbukwa Februari 2021 Waziri Jafo alikutana na wadau
wanaojishughulisha na uchimbaji mchanga katika mkoa huo kujadili changamoto za
kimazingira zinazotokana na uchimbaji mchanga kiholela kiholela katika mito na
mabonde ili kuweka utaratibu mzuri.
Kikao hicho kiliwezesha kuandaliwa Mwongozo wa
usafishaji mito utakaotumika katika Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kuondoa
mchanga, taka ngumu na tope ili kupunguza au kuondoa madhara ya mafuriko ambao
ulitolewa kwa mujibu wa kifungu cha 57 (2) cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira
ya mwaka 2004.
No comments:
Post a Comment