Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi Ameshiriki Katika Maziko ya Marehemu Sheikh Ali Rijali Kijiji cha Bambi Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa sita kushoto) akijumuika na Viongozi na Waislamu katika swala ya maiti ya  Marehemu Sheikh Ali Rijali  katika msikiti wa Ijumaa Bambi ambapo  amezikwa katika Kijiji kwao  Bambi Wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akitia udongo kama ishara ya kumzika Marehemu Sheikh Ali Rijali alipojumuika na Viongozi,Waislamu na Wananchi mbali mbali waliohudhuria katika maziko ya Sheikh Rijali yaliyofanyika leo  Kijiji kwao  Bambi Wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi na Wanafamilia ya Marehemu Sheikh Ali Rijali mara alipowasili katika msikiti wa Ijumaa Bambi kwa ajili ya kuswalia Mwili wa marehemu huyo aliyefariki na kuzikwa katika Kijiji cha Bambi Wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.