Habari za Punde

Wakazi wa Kaselya Wilayani Iramba Wanufaika na Mradi wa Maji

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (kushoto) alipata maelezo ya Mradi wa Maji Kaselya, kutoka kwa Diwani wa Kata ya Kaselya, Wilayani Iramba mkoani Singida, Mhe. Juma Makaula, alipotembelea na kukagua mradi huo ambao umekamilika na umeanza kutoa huduma kwa wananchi.

Na Benny Mwaipaja, Singida

WAKAZI wa Kata ya Kaselya Wilayani Iramba mkoani Singida wameondoka na na adha ya maji baada ya kukamilika kwa mradi wa Maji wa Kaselya uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 770.

Wakazi hao wameishukuru Serikali kwa kufanikisha na kukamilisha ujenzi wa mradi huo, wakati wa ziara ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, alipotembelea na kukagua mradi huo ambao fedha zake zinatokana na mradi wa kukabiliana na athari za UVIKO 
19.

“Tunakuomba utupelekee salam nyingi kwa Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kututatulia changamoto ya maji kafika kata yetu, ametutua ndoo kichwani wanawake na wewe Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wetu kwa jitihada zako za kufanikisha mradi huu na miradi mingine” walisema wakazi wa kata hiyo

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba aliahidi kumfikishia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pongezi za wananchi hao kwa jitihada zake za kuwaletea wananchi maendeleo kwa kasi kubwa.

Alisema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akipigiwa mfano na mashirika ya Fedha ya Kimataifa na nchi mbalimbali duniani kwa ubunifu mkubwa wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotokana na Fedha za mkopo usiokuwa na riba wa Benki ya Dunia wa shilingi trilioni 1.3 kwa ajiii ya  kukabiliana na athari za kiuchumi zinazotokana na changamoto ya UVIKO 19.

Aidha, aliwataka wananchi hao kutunza ipasavyo miundombinu ya mradi huo wa maji ili iweze kudumu muda mrefu na kuendelea kutoa huduma ya maji kwa wananchi.

Akiwa jimboni, Dkt. Nchemba ametembelea na kukagua ujenzi wa miradi mbalimbali ukiwemo ujenzi wa miundombinu ya madarasa  ya shule ya Sekondari Ndulungu, kituo cha afya Mwandegembe, Shule ya Sekondari Mbelekese, Kituo cha Afya Urugu na kuzungunza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika tarafa  ya Ndago.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiangalia miundombinu ya Mradi wa Maji Kaselya, ulioko wilayani Iramba, mkoani Singida,  alipotembelea na kukagua mradi huo ambao umekamilika na umeanza kutoa huduma kwa wananchi.
Waziri wa Fedha na Mipano, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Tarafa wa Tarafa ya Wilayani Iramba mkoani Singida, alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ukiwemo mradi wa maji wa Kaselya.
Waziri wa Fedha na Mipano, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (wa pili kulia), akikagua ujenzi wa miundombinu ya  madarasa ya shule ya Sekondari Ndulungu, iliyoko Wilayani Iramba mkoani Singida, alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ukiwemo mradi huo.
Waziri wa Fedha na Mipano, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na wakazi wa Kata ya Ndulungu, baada ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya  madarasa ya shule ya Sekondari Ndulungu, iliyoko Wilayani Iramba mkoani Singida, alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ukiwemo mradi huo.

Waziri wa Fedha na Mipano, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na wakazi wa Kata ya Kaselya, baada ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya  mradi wa maji Kaselya, ulioko Wilayani Iramba mkoani Singida, alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ukiwemo mradi huo.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango, Singida)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.