Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary
Senyamule akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika
katika ukumbi wa Jengo la Mkapa. Mhe. Senyamule ametangaza Kampeni Maalumu ya
upandaji miti katika Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kuikijanisha Dodoma.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na wadau wa mazingira, leo tarehe 30 Desemba 2022, imetangaza kampeni maalumu ya upandaji miti katika Mkoa wa Dodoma lengo hasa likiwa ni kutimiza lengo la kampeni ya kuikijani Dodoma.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa
wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipokua akizungumza na waandishi wa Habari
kwenye ukumbi uliopo kwenye jengo la Mkapa, ofisini kwake.
“Sote tunafahamu kuwa msimu wa
mvua umeanza hivyo, ni wakati sahihi kwa wananchi na wakazi wote wa Dodoma
kutekeleza kwa vitendo Kampeni ya upandaji miti kuanzia ngazi ya Kaya, Kata,
Vijiji, Vitongoji hadi ngazi ya Taasisi
na msisitizo wa mwaka huu ni kwamba miti yote itakayopandwa hakikisheni inakua
na kustawi vizuri” Amesisitiza Mhe. Senyamule
Kadhalika, Mkuu wa Mkoa
amezitaja baadhi ya faida za uwepo wa miti ya kutosha katika mazingira yetu na
Mkoa kwa ujumla kuwa ina mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi na jamii kwa
ujumla kwani misitu inatoa asilimia 45 ya malighafi za ujenzi, hunyonya hewa
ukaa, hutupatia hewa safi, kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji na pia
huchangia ongezeko la pato la Taifa.
“Ninafahamu wenzetu wakala wa
misitu TFS wamezalisha miche ya miti ya kutosha pale katika kitalu cha miti eneo
la Mailimbili na miche hiiinagawiwa bure, hivyo natoa rai kwa wanadodoma kufika
pale kuchukua miche ya miti na kupanda katika maeneo yenu. Tutapita kukagua
kila nyumba na kuona miti mitano iliyopandwa na wale wasiopanda watachukuliwa
hatua kwa kuwa hii ni sehemu yasheria ndogo tulizonazo kwenye Halmashauri”
Ameongeza Mh. Senyamule
Kampeni ya upandaji miti Mkoa
wa Dodoma inayotarajiwa kuanza Desema 31hadi msimu wa mvua utakapokwisha,
imelenga Halmashauri zote nane za Mkoa kwani lengo kuu la Mkoa ni kila Halmashauri
kupanda miti 1,500,000 kwa mwaka licha ya baadhi ya maeneo kupewa kipaombele
kama eneo la Ihumwa kwenye chanzo cha maji cha DUWASA na katika bonde la
Mzakwe.
No comments:
Post a Comment