Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akikata keki kama ishara ya kumbukizi ya kuadhimisha siku ya
kuzaliwa kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla iliyofanyika katika
Ukumbi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro – Swaswa. Kiasi cha shilingi Milioni
92.8 zimepatikana katika hafla ya kuchangia gharama za masomo wanafunzi wenye
uhitaji takriban 1,128 kutoka mikoa 26 ya Tanzania bara.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akikata keki kama ishara ya kumbukizi ya kuadhimisha siku ya
kuzaliwa kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla iliyofanyika katika
Ukumbi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro – Swaswa. Kiasi cha shilingi Milioni
92.8 zimepatikana katika hafla ya kuchangia gharama za masomo wanafunzi wenye
uhitaji takriban 1,128 kutoka mikoa 26 ya Tanzania bara.
Mkuu wa Mkoa
wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza katika katika hafla ya kumbukizi
ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika
katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro – Swaswa. Kiasi cha
shilingi
Milioni 92.8 zimepatikana katika hafla ya kuchangia gharama za masomo wanafunzi
wenye uhitaji takriban 1,128 kutoka mikoa 26 ya Tanzania bara. Wanafunzi hao ni
wa ngazi ya Astashahada, Stashahada na Shahada)
Mkoa wa Dodoma umeadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha matukio makubwa matatu ya kimkakati ambayo yameweka kumbukumbu ya kudumu kwa jamii na matokeo chanya
Matukio hayo ni pamoja na
changizo la kugharamia wanafunzi wenye mahitaji maalumu, uzinduzi kwa kituo
jumuishi kwa manusura wa ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto
kilichopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na zoezi la upandaji
miti.
Kiasi cha shilingi Milioni
92.8 zimepatikana katika chakula cha hisani kilichoandaliwa maalumu kusheherekea
siku ya kuzaliwa ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya kuchangia
gharama za masomo wanafunzi wenye uhitaji takriban 1,128 kutoka mikoa 26 ya
Tanzania bara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule katika hafla ya kuchangia Mfuko wa Kichungaji
wa Elimu Mtwara (Mtwara Pastoral Education Fund - MPEF) ametoa rai kwa
jamii kuhakikisha wanawezesha wanafunzi wahitaji kusoma ili kufikia ndoto zao.
Katika hafla hiyo Mhe. Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amechangia kiasi cha Shilingi Milioni 50 huku
milioni 42.8 zikichangwa na wageni walioalikwa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Mhe. Rosemary Senyamule amezindua
kituo cha utoaji huduma jumuishi kwa manusura wa ukatili wa kijinsia na ukatili
dhidi ya watoto kilichopo hapa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Akizindua
kituo hicho Mhe. Senyamule amesema Mkoa wa Dodoma ni kati ya Mikoa yenye
changamoto za matukio ya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya Watoto, hivyo
kituo hicho cha kwanza katika Mkoa kitasaidia manusura wa ukatili ambao watapata
huduma zote kwa haraka kwa wakati muafaka.
Amesema lengo la
kuanzishwa kwa kituo hicho ni kurahisisha mfumo wa rufaa kwa manusura katika
kupata huduma maalumu zingine kama vile huduma za afya, Ustawi wa Jamii na
huduma za msaada wa kisheria.
“Hakikisheni kituo
hiki kinafanya kazi masaa 24 ili kurahisha huduma na kutumiza malengo ya uanzishwaji
wake” Alisisitiza Mhe. Senyamule.
Awali Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma alijumuika na jumuiya ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) katika
zoezi la upandaji miti takribani 400 katika eneo la Vikonje ambapo makao makuu
ya TBC yanajengwa.
No comments:
Post a Comment