Habari za Punde

Bodi ya Wakala wa Uwezeshaji Wananchi kiuchumi yapongezwa


 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na  Bodi ya Wakala wa Uwezeshaji Wananchi kiuchumi na uongozi wake waliofika kijitambulisha Ofisini kwake Vuga.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameipongeza Bodi ya Wakala wa Uwezeshaji Wananchi kiuchumi na uongozi wake kwa kutekeleza kajukumu yao kwa mafanikio makubwa.

 

Mhe. Hemed ametoa Pongezi hizo alipokutana na kufanya mazungumzo na Bodi hiyo Ofisini kwake Vuga Jijini Zanzibar. 

 

Amesema ni muda mchache tokea kuanzishwa kwa Wakala huo ambapo wameanza kutekeleza dhamira ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ya kuwawezesha wanchi kupata mitaji na kutoa fursa za  kukuza uchumi na kupunguza changamaoto zinazoikabili jamii.

 

Amesema ni vyema kwa wakala huo kuanzisha mifumo ya kieletroniki katika shughuli za uendeshaji ili kuweza kutoa huduma bora Zaidi  na gharama nafuu kwa wananchi.

 

Aidha Mhe. Hemed ameridhishwa na utendaji kazi wa wakala kwa kufanya kazi  kwa kushirikiana  na Sekta binafsi na washirika wa maendeleo  ndani na nje ya nchi katika utafutaji na upatikanaji wa rasilimali fedha.

 

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya wakala wa Uwezeshaji Wananchi kiuchumi Ndg. Juma Amour Mohammed amemueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa baada ya kuchaguliwa kwa Bodi hiyo wameweza kutayarisha muundo wa taasisi pamoja na kuandaa mpango mkakati na kuratibu upatikanaji wa rasilimali fedha.

 

Aidha ameeleza kuwa Bodi inaendelea na mazungumzo na wadau mbali mbali wa Maendeleo kwa lengo la kukuza sekta ya Uwezeshaji nchini.

 

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa wakala wa uwezeshaji wa wananchi kiuchumi Ndg. Juma Burhan amesema kuwa  jumla ya wananchi 17,665 wamenufaika na fedha za uwezeshaji kati ya hao 8686 kutoka unguja wakiwemo wanaume 3311 na wanawake 5375 aidha kwa upande wa Pemba jumla ya wananchi 8979 wamenufaika wakiwemo wanaume 3425 na wanawake 5554.

 



Wakati wa mchana Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amejumuika na waumini wa Masjid JUMUIYA YA WAARABU..RAHA LEO katika Ibada ya Swala ya Ijumaa na kuwataka waumini hao kudumisha Umoja na Ushirikiano katika jamii ili kudumisha upendo kwa Wazanzibari.

Mhe Hemed amewataka wafanya biashara kuwa na Imani na uadilifu katika biashara zao kama ilivyoelekezwa katika kitabu kitukufu cha qur-an juu ya ufanyaji wa biashara na faida zake.

 Amesema kufanya hivyo kutapelekea  wananchi kuwa na Imani na wafanya biashara pamoja na Serikali yao amabayo imetoa muungozo juu ya ufanyaji wa biashara nchini.

………………………………………….

Abdulrahim Khamis

Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

10/02/2023

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.