Habari za Punde

Waziri Mkuu Mhe.Majaliwa Akabidhi Sadaka kwa Watoto wa Kituo cha Yatima Mwandaliwa Jijini Dar es Salaam

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhi sadaka ya mbuzi na vitu mbalimbali kwa watoto Husna Issa (kulia) na  Shaban Maulid  (wa tatu kulia) wa kituo cha kulea watoto yatima cha Mwandaliwa kilichopo Mbweni jijini Dar es salaam, Februari 17, 2023. Kushoto ni mwanae, Majaliwa Kassim na wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa kituo hicho, Haji Mahmoud.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Haji Mahmoud ambaye ni Mkurugenzi wa kituo cha kulea watoto yatima  cha Mwandaliwa kilichpo Mbeni jijini Dar es salaam wakati alipokagua mabweni ya kituo hicho,
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea risala kutoka kwa watoto wa kituo cha  kulea watoto yatima cha Mwandaliwa, Husna Issa (kushoto) na Shaban Maulid wakati alipotembelea kituo hicho kilichopo Mbweni jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipotembelea kituo cha kulea watoto yatima cha Mwanadaliwa kilichopo Mbweni jijini Dar es salaam, Februari 17, 2023.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.