Habari za Punde

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan azindua Mradi wa Minara ya kurusha Matangazo ya Televisheni Ardhini, DTT, ya Kampuni ya Azam Media Ltd, Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuashiria ufunguzi wa Mradi wa Minara ya kurusha matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni ya Azam Media kwenye hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya Ofisi hizo zilizopo Barabara ya Mandela Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuashiria ufunguzi wa Mradi wa Minara ya kurusha matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni ya Azam Media kwenye hafla iliyofanyika katika Makao Makuu ya Ofisi hizo zilizopo Barabara ya Mandela Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited Ndugu Tido Mhando wakati alipotembelea Studio za matangazo za Azam TV zilizopo Barabara ya Mandela Jijini Dar es Salaam Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited Ndugu Tido Mhando wakati alipotembelea Studio za matangazo za Azam TV zilizopo Barabara ya Mandela Jijini Dar es Salaam 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya King’amuzi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Ndugu Abubakar Said Salim Bakhresa kwa ajili ya kuangalia maudhui mbalimbali ya Azam TV mara baada ya kuzindua mradi wa Minara ya kurusha matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni hiyo kwenye hafla iliyofanyika katika Ofisi zao zilizopo Barabara ya Mandela Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na Wafanyakazi wa Azam Media mara baada ya kufungua Minara ya kurusha matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni hiyo kwenye hafla iliyofanyika katika Ofisi za Kampuni hiyo zilizopo Barabara ya Mandela Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Mtoto Georgina Magesa (8) mara baada ya kuonana na Mhe. Rais katika Ofisi za Azam Media zilizopo katika Barabara ya Mandela Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Mtoto Georgina Magesa (8) mara baada ya kuonana na Mhe. Rais katika Ofisi za Azam Media zilizopo katika Barabara ya Mandela Jijini Dar es Salaam.

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Tuzo kwa Niaba ya Kampuni ya Azam Media Mama Violet Maro Mwanamke wa kwanza Mwandamizi katika fani ya Habari nchini wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa Minara ya kurusha matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni ya Azam Media Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Tuzo kwa Niaba ya Kampuni ya Azam Media Mama Debora Mwenda Mtangazaji wa kwanza Mwanamke kuandaa vipindi vya Watoto  wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa Minara ya kurusha matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni ya Azam Media Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Tuzo kwa Niaba ya Kampuni ya Azam Media Bi Hadija Said Mtangazaji wa kwanza Mwanamke nchini akihudumu katika Redio ya Taifa (RTD) wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa Minara ya kurusha matangazo ya Televisheni Ardhini (DTT) ya Kampuni ya Azam Media Jijini Dar es Salaam
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.