Mwenyekiti wa Kikao
cha Kamati ya Wataalamu wa wa Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na
Kuongeza Usalama wa Chakula (LDFS) unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais,
Waza Kiunsi akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kamati hiyo mara baada
ya kumaliza kwa kikao baina yao kilichofanyika katika Ofisi ya Makamu wa Rais
Mji wa Serikali, Mtumba Dodoma, tarehe 11 Mei, 2023.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Kikao hicho kilichofanyika katika
Ofisi za Makamu wa Rais, Mtumba Jijini Dodoma kilihudhuriwa na Wakurugenzi
Watendaji wa Halmashauri za Wilaya zinatekeleza Mradi wa LDFS kutoka Tanzania
Bara na Zanzibar ambapo pamoja na kupokea na kujadili taarifa hiyo, wajumbe wa
kikao hicho pia walipitisha bajeti ya Mradi kwa mwaka 2023/2024.
Kikao kilichoongozwa na Kaimu Mkurugenzi
wa Sera na Mipango kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Waza Kiunsi pia
kilipitia taarifa ya mradi na kupokea maoni, ushauri na mapendekezo kutoka kwa
wajumbe na namna bora ya utekelezaji wa bajeti ijayo ya mradi katika mwaka
2023/2024.
Mradi wa LDFS miongoni mwa miradi
kumi na mbili ya majaribio inayotekelezwa katika nchi kumi na mbili zilizopo
Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania. Fedha kwa ajili ya utekelezaji wa
Mradi huu zinatolewa na Mfuko wa Dunia wa Mazingira (GEF) kwa thamani ya Dola
za Marekani milioni 7.156 na kusimamiwa na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya
Kilimo.
Katika Tanzania Mradi wa GEF unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia Julai 2017 hadi Septemba 2022 katika Halmashauri za wilaya ya Kondoa Dodoma, Nzega (Tabora), Mkalama (Singida), Magu (Mwanza) na Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Zanzibar.
No comments:
Post a Comment