Habari za Punde

Ufunguzi wa Michuano ya Klabi Bingwa Mchezo wa Netiboli

Na Brown Jonas

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amewakaribisha wadau na wapenda michezo wa sekta binafsi wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika shughuli za michezo hususani mchezo wa Netiboli.

Mhe. Chana amesema hayo Juni 23, 2023 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua mashindano ya Klabu Bingwa ya Netiboli katika viwanja vya Netiboli, Benjamini Mkapa.

“Nitoe wito kwa wadau wengine zikiwemo taasisi mbalimbali za ndani na nje kuwekeza katika michezo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya kimichezo Pamoja na kugharamia shughuli za michezo hususani michezo ya wanawake pamoja na watu wenye ulemavu” amesema Mhe. Chana

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Dkt. Devota Marwa amesema kuwa wataendelea kuratibu programu mbalimbali za maendeleo ya mchezo huo.

Mashindano hayo yamelenga kuchochea ushindani na kupata timu bora ya taifa





 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.