Habari za Punde

Wananchi Watakiwa Kuendelea Kuiamini Serikali

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba akisikiliza maelezo kuhusu mfumo mpya wa ununuzi wa umma kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Taasisi ya Usimamizi ya Ununuzi wa Umma (PPRA), Bi. Zawadi Msala, alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini humo.

Na Farida Ramadhani, WF – Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba amewataka wananchi kuendelea kuiamini Serikali kwa kuwa mambo yote iliyoyapanga yatatekelezwa kikamilifu.

Ametoa rai hiyo alipotembelea na kuzungumza na washiriki wa banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini humo.  

Dkt. Mwamba alisema katika kipindi hiki cha utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali iliyosomwa hivi karibuni, Serikali itahakikisha inatekelezwa kiufasaha na kufukia malengo yaliyo kusudiwa.

Akizungumzia Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba jijini humo, aliwahamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi ili kupata elimu kuhusu masuala mbalimbali ya biashara na uwekezaji.

 

“Hapa ni kwa ajili ya biashara, viwanda na uwekezaji, kuna mengi ya kujifunza ambayo yatawezesha wananchi kujiinua kiuchumi”, alibainisha Dkt. Mwamba.

Alisema katika banda la Wizara ya Fedha, washiriki wanaari ya kuwahudumia wananchi hivyo watakapo tembelea maonesho hayo wasisite kupitia banda hilo muhimu katika kusimamia uchumi wa nchi.

“Washiriki wamejipanga na kwa namna wanavyotoa elimu ni rahisi mno kuwaelewa na kufanya maamuzi sahihi kutokana na elimu iliyopatikana” alifafanua Dkt. Mwamba.

Aidha, alionesha kufurahishwa na namna ambavyo wananchi wameonesha kufurahishwa na kuondolewa kwa tozo za miamala ya simu na kubainisha kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha inapunguza maumivu kwa wananchi.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba akizungumza na maafisa wa wizara hiyo, Bi. Jackline Kayuki(kushoto), Bw. Fronto Furaha (katikati) na Bw. Emmanuel Matiku, alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini humo.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba akifurahia jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Wakala wa Soko la Hisa la Dar es Salaam -Exodus Advisory, Bw. Ramadhani Kagwandi na Afisa Masoko wa Kampuni hiyo, Bi. Asha Mwinshehe, alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini humo.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa pili kushoto) akisikiliza maelezo kuhusu mafunzo yanayotolewa na Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) kutoka kwa Mkurugenzi wa Tafiti, Shauri za Kitaalam na Machapisho, Dkt. Gorah Abdallah alipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini humo. Wa kwanza kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo hicho, Prof. William Pallagyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba akisikiliza maelezo kuhusu wanufaika wa mikopo inayotolewa na Benki ya Maendeleo TIB, kutoka kwa Meneja wa Fedha za Uwakala wa banki hiyo, Bi. Monica Luziro, alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini humo.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara hiyo walioshirikili katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba, Barabara ya Kilwa, jijini humo, alipotembelea banda la Wizara hiyo.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango, Dar es Salaam)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.