Habari za Punde

Wanawake wapatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kujiajiri

Mkufunzi  Asha Abdalla Salim akiwaelekeza washiriki wa mafunzo ya kuwawezesha wanawake kiuchumi  kutengeneza pilipili ili kuweza kujiajiri,huko Skuli ya Mwembe makumbi Zanzibar.PICHA NA FAUZIA MUSSA- MAELEZO ZANZIBAR
Mkufunzi Bimkubwa Massoud  Ali akiwaelekeza washiriki wa mafunzo ya kuwawezesha wanawake kiuchumi  kutengeneza mafuta ya mgando  ili kuweza kujiajiri,huko Skuli ya Mwembe makumbi Zanzibar.PICHA NA FAUZIA MUSSA- MAELEZO ZANZIBAR

Meneja Shirika lisilo la Serikali la wanawake na Uchumi  wa Viwanda (WAUVI)  Thneyyu Mabrouk Hassan akizungumza machache na kumkaribisha Naibu Meya Mjini Khadija Ame kufungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake kujiajiri yaliyofanyika huko Skuli ya Muembe Mkaumbi Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Unguja.PICHA NA FAUZIA MUSSA- MAELEZO ZANZIBAR

Mkurugenzi   Shirika lisilo la Serikali la wanawake na Uchumi  wa Viwanda (WAUVI) Taifa Habiba Said Ngelite akizungumza na wanawake kuhusu ujasiriamali wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kujiajiri huko Skuli ya Muembe Mkaumbi Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Unguja.PICHA NA FAUZIA MUSSA- MAELEZO ZANZIBAR

 aibu Meya Baraza a Manispaa Mjini Khadija Ame akizungumza na wanawake kuhusu ujasiriamali wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kujiajiri huko Skuli ya Muembe Makumbi Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Unguja.PICHA NA FAUZIA MUSSA- MAELEZO ZANZIBAR


Rahma Khamis Maelezo    

Naibu Meya Baraza la Manispaa Mjini Khadija Ame amewataka wanawake kutumia fursa  mbalimbali za mafunzo zinapotokezea  zinazolenga kuwainua kiuchumi.

Akizungumza na wanawake hao katika Skuli ya Muembemakumbi wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kujiari amesema mafunzo hayo yatawasaidia kuwawezesha kujiajiri na  kujiletea maendeleo katika jamii.

Amesema kuna baadhi ya wanawake hawajishuhulishi na kitu chochote cha kuwaingizia kipato jambo linalorejesha nyuma jitihada za Serikali katika kupambana ili kuwawezesha kiuchumi.

Aidha amefahamisha kuwa  iwapo wanawake watajiunga na vikundi mbalimbali vya ujasiriamali  wataweza kujiongezea kipato  na kjiimarisha .

"Tumieni ujuzi wenu kujiinua kiuchumi kwani Serikali inatumia nguvu nyingi ikiwemo kuanzisha vikundi na  kuwapatia elimu ya ujasiriamali hivyo tuzienzi nguvu hizi ili tujiletee maendeleo "alisisitizia Naibu Meya

Amesema dhamira ya Serikali zote mbili  ni kuwainua wanawake kiuchumi hivyo aliwataka wanawake hao  kuyafanyia kazi mafunzo wanayopatiwa ili kujikwamua kimaisha.

"Ni jambo zuri la kujivunia  tunaona Viongozi wetu wanafanya kazi kubwa katika kuleta maendeleo ikiwemo kujenga  hospitali ,Barabara na viwanda ,hivyo lazima tusifu mazuri tunayofanyiwa kwani wao wako mstari wa mbele kuhakikisha wanawake wanaimarika kiuchumi "alifafanua Naibu .

Katika hatua nyingine Naibu Meya amefafanua kuwa Serikali kupitia Baraza la Manispaa Mjini wametenga kiasi cha sh, milioni 284 kwa ajili ya wananchi hasa wanawake na vijana ili kuwawezesha kiuchumi hivyo amewataka wanawake kushikamana ili kufikia malengo .

"Tuutajitahidi kadri ya uwezo wetu  kuhakikisha pesa hizo zinapatikana kwa ajili ya kuwainua wanawake kimaendeleo, "alifahamisha Naibu

Nae Mkurugenzii  Mkuu ambaye pia ni Mwanzilishi wa Shirika la wanawake na  Uchumi  wa Viwanda Tanzania  Halima Saidi Mngite amesema kuwa lengo la Shirika hilo ni kukuza viwanda ,kutoa mafunzo na kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Aidha amefahamisha kuwa wanatarajia kua na viwanda vingi  vya Wanawake wa Tanzania ikiwemo viwanda vya chumvi, asali na mafuta ili kusaidia Serikali kupunguza tatizo la ajira nchini.

Mkurugenzi ameeleza kuwa hatua ya kuanzisha shirika hilo linalofanya kazi  na Serikali kwa  kuwajengea uwezo wa kujitegemea ni baada ya kubaini kua wanawake wengi  wamekua tegemezi kwa familia na  Taifa kwa ujumla .

 Ameongeza kuwa wanawake wana mchango mkubwa katika jamii hivyo kupitia programu ya  Zunguka na Mama Samia  itasaidia kuwafikia wanawake wote Tanzania katika kuwapatia elimu ya kujiwawezesha kiuchumi.

Amefahamisha kuwa Serikali ya Muungano wa Tanzania inaaunga mkono juhudi za Shirika kutokana na kuona  Shirika hilo linapambana katika kuwainua wanawake kiuchumi .

"Tumuunge mkono mama Samia Suluhu  ili tusonge mbele kwani anaona juhudi zetu katika kuwapambania wanawake hivyo tuamke kwani maisha yamebadilika,tutoke  katika maisha ya utegemezi," akiwahimiza wanawake.

Nao washiriki wa mafunzo hayo wamesema mafunzo yatawasaidia kujiinua kiuchumi na kuwataka wanawake wenzao kuacha kutegemea wanaume na badala yake kujishughulisha ili kuleta maendeleo.

Shirika la Wanawake na Uchumi wa Viwanda ni Shirika lisilo la Kiserikali limeanzishwa mwaka 2000 na linajishughulisha na kuwawezesha wanawake kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.