Habari za Punde

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan azindua Miradi mbalimbali ya Maendeleo kuelekea kwenye Kilele cha Tamasha la Kizimkazi Zanzibar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi pamoja na viongozi wengine mara baada ya kufungua Madarasa 6 ya jengo la Skuli ya Msingi Muyuni B tarehe 29 Agosti, 2023 Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati akikagua Madarasa ya Shule ya Msingi Muyuni B mara baada ya ufunguzi katika Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar tarehe 29 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi wengine katika picha ya pamoja na Walimu wa Skuli ya Msingi Muyuni B mara baada ya ufunguzi kwenye Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar tarehe 29 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi wengine wakati akikata utepe kufungua Chumba cha Kompyuta na ukumbi wa Mtihani wa Skuli ya Sekondari ya Muyuni B kwenye hafla fupi iliyofanyika Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi tarehe 29 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza mara baada ya kufungua Chumba cha Kompyuta na ukumbi wa Mtihani wa Skuli ya Sekondari ya Muyuni B kwenye hafla fupi iliyofanyika Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar tarehe 29 Agosti, 2023 katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna kuhusu Ujenzi wa Skuli ya Maandalizi Tasani, Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar tarehe 29 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Skuli ya Maandalizi Tasani, Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar tarehe 29 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama wakati wa heshima ya Wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili kwenye Kituo cha Polisi Kizimkazi Mkunguni kwa ajili ya Ratiba ya kugawa magari kwa ajili ya Jeshi hilo Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 29 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuzindua ugawaji wa Gari la OCD Kizimkazi Mkunguni pamoja na Gari la OCD Makunduchi tarehe 29 Agosti, 2023 katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi funguo za magari Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad mara baada ya uzinduzi katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi funguo na gari la huduma katika Kituo cha afya cha Mama na mtoto Kizimkazi Dimbani tarehe 29 Agosti, 2023 katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua Kituo cha Afya cha mama na mtoto Kizimkazi Dimbani tarehe 29 Agosti, 2023 katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Kituo cha Afya cha mama na mtoto Kizimkazi Dimbani tarehe 29 Agosti, 2023 mara baada ya kukizindua katika shamrashamra za kuelekea kwenye kilele cha Tamasha la Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.