RAIS wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi
akihutubia katika hafla ya Ufunguzi wa Kituo cha Afya Bumbwini Makoba Wilaya ya
Kaskazini “B” Unguja leo 14-8-2023 na kukifungua rasmin Kituo hicho na kutowa
huduma ya Afya kwa Wananchi wa Bumbwini.
SERIKALI ya Mapinduzi ya
Zanzibar, imesema itaendelea kuimarisha huduma za afya ya msingi kwa maeneo yote ya
Unguja na Pemba ikiwa na lengo la kuboresha huduma za uzazi salama, matibabu ya
meno na kinywa, uchunguzi wa ‘ultra sound” na huduma za maabara zipatikane kwa
ufanisi wenye vituo vya afya vyote vya msingi kwa maeneo yote ya nchi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameyasema hayo kwenye ufunguzi wa kituo cha
Afya, Bubwini Makoba, Wilaya
ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Alisema, Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu,
upatikaji wa dawa muhimu, vifaa tiba, na
rasilimali watu ikiwemo madaktari, wauguzi, wafamasia na wataalamu wengine
muhimu wanaohitajika katika sekta ya afya.
Aidha, Dk. Mwinyi alieleza azma ya Serikali
kujenga nyumba za wafanyakazi kwa baadhi ya hospitali za Wilaya, Unguja na
Pemba ili kupunguza tatizo la makaazi kwa watumishi wa sekta ya afya na
kuwafanya wabakie kwenye vituo vyao vya kazi muda wote ili waendee kutoa huduma
hasa kwa kesi za dharura.
Alieleza, hatua hiyo itaboresha zaidi
mfumo wa rufaa na kupunguza kwa kiasi kikubwa kasi ya wagonjwa kwenda Hospitali
ya Mnazi Mmoja na kupunguza mrundikano wa wagonjwa Mnazi mmoja.
Dk. Mwinyi alisema, licha ya kuwepo kwa baadhi
ya changamoto kwenye sekta ya Afya zikiwemo uhaba wa wafanyakazi mabingwa na
wabobezi kwenye kada mbali mbali za Afya, hali aliyoielezea inaisababishia
Serikali kutumia fedha nyingi kwa matibabu ya wananchi nje ya Zanzibar.
Rais Dk. Mwinyi, alieleza katika kukabiliana
na hali hiyo, Serikali imeamua kushirikiana na sekta binafsi ambao wataendelea
kuhudumia hospitali za Serikali zikiwemo huduma za uchunguzi wa maradhi hasa kwa maeneo yaliyoimarika kwenye utekelezaji
wake.
Alisema nia ya
Serikali ni kufikia malengo iliyojipangia ya kuwahikishia wananchi wake huduma
nzuri ndani ya wakati unaotakiwa kwenye hospitali na vituo vyote vya Afya vya
maeneo yote nchini.
“Nimeamua kulieleza hili kwa vile kuna
baadhi ya watu kwa makusudi wameanza kupotosha na kuwadanganya wananchi, utaratibu
huu umeanza kutumika kwa mafanikio katika hospitali ya Mnazi Mmoja na
utaendelezwa kwenye hospitali zetu zote za Wilaya pamoja na hospitali ya Mkoa
ya Lumumba iliopo Mkoa wa Mjini Magharibi” Alibainisha Dk. Mwinyi.
Katika hatua nyengine, Rais Dk. Mwinyi
aliwaagiza watumishi wote watakapelekwa
kufanya kazi kituo cha Afya Bumbwini Makoba wajitahidi kuitunza miundombinu
iliyopo, kufanyakazi kwa moyo wa kujitolea na huruma kwa wagonjwa na kuzingatia
maadili ya kazi zao na kutumia lugha nzuri kwa wagonjwa watakaowahudumia.
Akizungumza kwenye
hafla hiyo, Waziri wa Afya, Nassor Ahmeid Mazrui alisema, ujenzi wa kituo
hicho ni utekelezaji wa juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuimarisha
vituo vya Afya vya msingi nchi nzima ili kuboresha huduma za Afya sambamba na
ujenzi wa hospitali 11 zikiwemo 10 za Wilaya na moja ya Mkoa.
Naye,
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dk. Amour Suleiman, alisema Ujenzi wa
kituo hicho ulianza May 14 mwaka 2022 na kukamilika mwezi June mwaka huu
ambao umegharimu shilingi milioni 450,
770, 400 hadi kukamilika kwake ambapo huduma za kliniki mbalimbali zinatolewa
na kituo hicho ikiwemo huduma za mama wajawazito na watoto, maabara na
ultrasound, vifaa tiba, meno, uangalizi maalum, mashine za kisasa za
kupimiamagonjwa yasiyoambukiza ikiwemo presha, sukari na mashine za kupimia
umeme wa moyo.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment