Habari za Punde

Makatibu Wakuu wa SMT na SMZ Wakutana Kujadili Masuala ya Muungano

Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) Balozi Dkt. Moses Kusiluka akiongoza kikao cha Makatibu Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kujadili masuala ya Muungano kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Septemba, 2023. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed Said.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga (kulia) akifuatilia kikao cha Makatibu Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kujadili masuala ya Muungano kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam
Naibu Makatibu Wakuu Ofisi ya Makamu wa Rais, kulia ni Bw. Abdallah Mitawi – Muungano na Dkt. Switbert Mkama - Mazingira (wa pili kulia) wakifuatilia kikao cha Makatibu Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kujadili masuala ya Muungano kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam
Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakifuatilia kikao cha cha Makatibu Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kujadili masuala ya Muungano kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam 


Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw. Ali Juma wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kujadili masuala ya Muungano kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam 
Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Mitawi (katikati) akifurahia jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi, Bw. Xavier Daudi kabla ya kuanza kwa kikao cha Makatibu Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kujadili masuala ya Muungano kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam 
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) Balozi Dkt. Moses Kusiluka (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Mhandisi Zena Ahmed Said (wa pili kulia), Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga na Makatibu Wakuu kutoka SJMT na SMZ mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kujadili masuala ya Muungano kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam 
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) Balozi Dkt. Moses Kusiluka (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Mhandisi Zena Ahmed Said (wa pili kulia), Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kujadili masuala ya Muungano kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.