Habari za Punde

Maofisa IT na Utumishi Watakiwa Kukamilisha Usajili wa Wafanyakazi katika Mfuko wa Huduma ya Afya

Baadhi ya Maafisa Utumishi na IT wa Serikali wakifuatilia mkutano wa mrejesho wa usajili wa Wafanyakazi katika mfumo wa Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar uliofanyika katika Ukumbi wa Studio Rahaleo Wilaya ya Mjini Unguja leo 22-9-2023.

 

Picha na Rahma Khamis Maelezo

Na Rahma Khamisi Maelezo.                      22/9/2023

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar, (ZHSF) Yassir Ameir Juma amewataka wafanyakazi wa Taasisi za Serikali kukamilisha usajili wa  huduma za afya kwa haraka ili kupatiwa kadi za uwanachama.

 

Wito huo ametolewa katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo wakati wa Kikao cha mrejesho wa usajili wa uwanachama wa Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar kwa Maafisa Utumishi na IT wa Serikali.

 

Amefahamisha kuwa jumla ya wanachama 26 elfu wameshasajiliwa rasmi ambapo wafanyakazi 20 hawajakamilisha usajili huo hivyo amewahimiza kukamilisha usajili wao ili kuanza kutumia huduma hiyo.

 

Aidha amesema kuwa  Mfuko  una haki ya kuhakikisha wanachama wote wamesajiliwa katika mfumo  na kupata huduma zote za msingi,

 

Amesema kwa wafanyakazi walikwisha kamilisha usajili wao watapatiwa kadi zao  hivi karibuni 

 

Kaimu Mkurugenzi ameongeza kuwa kwa wale ambao wameshakamilisha usajili wao watapatiwa ujumbe mfupi kupitia simu zao kuhakikisha usajili wao  hivyo kila mtu ahakikishe anapata taarifa zake ili kuwaondeshea usumbufu wanachama wao.


Nae Afisa Tehama kutoka Wizara ya Fedha Muhammed Abdalla Ali amesema kuwa lazima wafanyakazi wote wa serikali  wawemo katika mfuko wa huduma ya afya  ili kurahisisha kuonekana kadi inapoingizwa  katika mfumo huo.

 

Aidha amefahamisha kuwa katika mfumo huo kutakuwa na invoice ambayo  itaonesha kila mfanyakazi na taarifa zake ili kuondosha usumbufu.

 

 "Ikitokea  katika mfumo wako kuna watu 20 na invoice yako inaonesha watu 21 hapo utatakiwa  kutoa taarifa sehemu husika kwa ajili ya kurekebishiwa," alifahamisha.

 

 Nao wafanyakazi hao wameuomba  Mfuko huo kuwapatiwa taarifa  za uhakika pindi watakapokamilisha usajili nili kuweza kutambua kinacoendelea.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.