Habari za Punde

Walimu wakuu na washika fedha wapatiwa mafunzo maalum ya kuisimamia na kutunza kumbukumbu ya matumuzi ya fedha

Baadhi ya Walimu Wakuu wa  na washika fedha wa Skuli za Sekondari Unguja wakiwa kwenye mafunzo maalum ya kuisimamia na kutunza kumbukumbu ya matumuzi ya fedha ukumbi wa mikutano Skuli ya Dk Ali Mohamed Shein Wilaya ya Mjini Unguja.
 
Baadhi ya Walimu Wakuu wa  na washika fedha wa Skuli za Sekondari Unguja wakisikiliza kwa makini kwenye mafunzo maalum ya kuisimamia na kutunza kumbukumbu ya matumuzi ya fedha ukumbi wa mikutano Skuli ya Dk Ali Mohamed Shein Wilaya ya Mjini Unguja.
Mkurugenzi Idara ya Elimu Sekondari Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar bi Asya Iddi Issa alipokuwa akitoa mada kwenye ufunguzi wa Mafunzo kwa Walimu Wakuu na washika fedha wa Skuli za Sekondari Unguja Katika ukumbi wa mikutano Skuli ya Dk Ali Mohamed Shein Wilaya ya Mjini Unguja.
 

Mkurugenzi Idara ya Elimu Sekondari Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar bi Asya Iddi Issa amesema kupewa Mafunzo ya kuisimamia na kutunza kumbukumbu ya matumuzi ya fedha kutawasaidi kutimiza majukumu yao.
Hayo ameyasema Leo Tarehe 10/09/2023 wakati wa kufungua Mafunzo kwa Walimu Wakuu na washika fedha wa Skuli za Sekondari Unguja Katika ukumbi wa mikutano Skuli ya Dk Ali Mohamed Shein Wilaya ya Mjini Unguja.
Amesema Mafunzo hayo kwa Walimu kutawasaidia na kuweza kufata utaratibu wa uhalali wa matumuzi ya fedha kwa kila mwaka.
Pia aliwasisitiza washika fedha hao kuhakikisha wanatunza risiti za matumuzi katika Skuli zao kwani ndio njia itakayoonesha matumizi ya fedha za Serikali.
Bi Asya amewasisitiza kuhakikisha wanapitia ripoti ya Mkaguzi wa hesabu wa wizara na kuyafanyia kazi mapungufu yatakayojitokeza.
Aidha Mkurugenzi amesisitiza kuelekea mtihani wa Taifa ni lazima kila skuli ijiandae na kuwaandaa wanafunzi kuja kukabiliana na mitihani hiyo na kuja kupata matokeo mazuri mwisho wa mwaka.
Mapema akiwasilisha hoja zilizojitokeza katika ukaguzi wa Skuli za Unguja na Pemba Mkaguzi wa hesabu za ndani Wizara ya Elimu Zanzibar bwana jabir Kipenda jabir amesema Walimu Wakuu anawajibu wa kuhakikisha matumizi yote yanayofanyika katika Skuli yake anayajua kwa kuwa na ithibati ya uingiaji wake na utokaji wake.
Aidha amewataka kuhakikisha wanapotaka vifaa wafate utaratibu wa kuandika barua ili kupata uhalali wa watumizi wa vifaa bila ya kuleta mashaka.
Nae Mhasibu wa wizara Ali Rajab alitoa maelekezo kwa washika fedha hao juu ya jinsi ya kufunga na kuweka uwiano wa fedha kila mwezi. Mkurugenzi alisisitiza zaidi kufuatwa taratibu na sheria za fedha zilizotolewa na Serikali kupitia Wizara ya fedha.
Mafunzo hayo ya siku moja yamewashirikisha Walimu Wakuu na washika fedha wa Skuli za Sekondari Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.