Habari za Punde

Benki ya Maendeleo TIB Yaadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Robert Ndaki (katikati) akikata keki na baadhi ya wateja na wafanyakazi wa benki hiyo kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja 2023 katika hafla fupi iliyofanyika katika Makao Makuu ya Benki ya Maendeleo TIB, Jijini Dar es Salaam. 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Robert Ndaki (katikati) na baadhi ya wateja na wafanyakazi wa benki hiyo wakionesha keki zenye ujumbe wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2023 katika hafla fupi iliyofanyika katika Makao Makuu ya Benki ya Maendeleo TIB, Jijini Dar es Salaam. 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Robert Ndaki (katikati) akimpa zawadi mmoja wa wateja wa benki hiyo, Dk. Ameir Binzoo ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Vifaa Tiba cha Msagara Investment, kilichopo Bagamoyo mkoa wa Pwani. 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Robert Ndaki (kulia) akimpa zawadi Bw. Ravi Badhari (kushoto), mmoja wa wawakilishi wa wateja kutoka Kampuni ya PIPES. 
Meneja Uhusiano na Masoko wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Saidi Mkabakuli akitoa neno la shukran mara baada ya kukamilika kwa tukio la kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja 2023 katika hafla fupi iliyofanyika katika Makao Makuu ya Benki ya Maendeleo TIB, Jijini Dar es Salaam.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.