Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Akihutubia na Kulifungua Kongamano la Pili la Kimataifa la Usimamizi wa Biashara na Maendeleo ya Uchumi

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla akitembelea maonesho katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Pili la Kimataifa la Usimamizi wa Biashara na Maendeleo ya uchumi lililofanyika katika Ukumbi wa hoteli hiyo Jijini Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Dkt. Saada Salum Mkuya akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmin Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla, kulifungua Kongamano la Pili la Kimataifa la Usimamizi wa Biashara na Maendeleo ya uchumi lililofanyika katika Ukumbi wa Hotel Verde Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla akimkabidhi Cheti cha Shukrani kwa Muwakilishi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) wakati wa hafla ya ufunguzi wa kongamano la Pili la Kimataifa la Usimamizi wa Biashara na Maendeleo ya uchumi lililofanyika katika Ukumbi wa Hotel Verde Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla akihutubia na kulifungua Kongamano la Pili la Kimataifa la Usimamizi wa Biashara na Maendeleo ya uchumi lililofanyika katika Ukumbi wa Hotel Verde Zanzibar.

Na.Mwandishi OMPR.                                                                                                                           
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zitaendelea kuwekeza katika kujenga mazingira wezeshi ili kuweza kuwa na chumi imara unaojumuisha Sekta rasmi na zisizo rasmi nchini.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussen Ali Mwinyi ameyasema hayo katika hutuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla katika hafla ya ufunguzi wa kongamano la Pili la Kimataifa la Usimamizi wa Biashara na Maendeleo ya uchumi lililofanyika katika Ukumbi wa Hotel Verde Zanzibar.

Amesema kuwa ili kuweza kuwa na uchumi Imara Serikali zote mbili  zinafanya uwekezaji mkubwa katika miundombinu mbali mbali ikiwemo ujenzi wa barabara, reli, madaraja ya kisasa, Bandari na viwanja vya ndege pamoja na miundombinu mengine ambayo ni nguzo muhimu katika kukuza biashara.

Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa nchi haiwezi kuendelea   kwa kutegemea ubunifu unaotoka  Mataifa yaliyoendelea katika ulimwengu wa sasa wenye ushindani wa kibiashara hivyo ni lazima tuwekeze na kuzitumia tafiti zetu katika kutatua chamgamoto zinazoikabili jamii yetu.

Amesema kuwa serikali zinaendela kufanya juhudi za kukabiliana na chamgamoto ya ukuaji wa uchumi hasa katika kuhakikisha kuwa sekta binafsi inakuwa na mchango mkubwa katika ukuwaji wa uchumi na kuwataka watafiti kufanya tafiti ambazo zitaonesha namna bora ya kuboresha mazingira ya biashara na kutoa ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili wafanyabiashara pamoja na wananchi kwa ujumla.

Rais Dkt Mwinyi amesema kasi ya ukuaji wa uchumi ni wastani wa asilimia 5.2 katika robo tatu ya kwanza ya mwaka 2022 kwa Tanzania bara na 5. 4 kwa upande wa Zanzibar kulikotokana na jitihada za kuimarisha uchumi wa buluu, kuimarika kwa  shuhuli za utalii na sera madhubuti za fedha na kibajeti.

Amewataka wanataaluma na watafiti kulitumia  kongamano hilo katika kubadilishana uzoefu na watafiti wa nchi za nje ili kuchota uzoefu na ujuzi ambao utakuja na suluhisho endelevu kwa changamoto zetu na kuepusha kuendelea kutumia tafiti za nje ambazo nyingi siyo sahihi kwa mazingira, teknolojia na historia ya nchi yetu.

Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mje. Dkt Saada Mkuya Salum ameipongeza Wizara ya Fedha ya Tanzania kwa uamuzi wa Kongamono hili kufanyika Zanzibar ambalo litatoa fursa kwa washiriki kubadilishana uzoefu katika usimamizi wa fedha, kufanya tafiti zenye ubunifu na kutafakari namna ya kukuza uchumi wa nchi na taifa kwa ujumla.

Amesema kuwa Zanzibar imeanzisha Taasisi ya wahasibu, wakaguzi, wasimamizi na washauri wa kodi (ZIATC) ambapo ameitaka Taasisi ya ya uhasibu Tanzania (TIA)  kujenga ushirikiano na Taasisi ya ZIATC  ili kuzidi kukuza na kuimarisha Uchumi wa Taifa.

Kwa upande wake mtendaji mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Professor William Pallangyo amesema kuwa kupitia kongamano hili kutaibua mbinu mbali mbali kutoka kwa wataalamu wa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kukuza uchumi wanchi.

Amefahamisha  kuwa uchumi endelevu ni kiungo kikubwa katika nchi kinachowasaidia wananchi kupiga hatua kutoka sehemu moja kwenda nyengine hivyo ni lazima seriakli kuhakikisha kunakuwepo  utawala bora wenye kufuata sheria ili kuweza kufikia malengo na mikakati ya  kukua kwa uchumi nchini.

Nao watoa mada katika kongamano hilo wamesema lengo la kukutana kwao ni kubadilishana uzoefu katika masuala ya kiuchumi jambo ambalo litaweza  kuisaidia serikali katika kupambana na umasikini na kukuwa kwa uchimi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Akiwasilisha maada kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu Dkt. Auric Kubuli amesema Sekta ya Uchumi wa Buluu ni muhimu sana kwa Uchumi na Maendeleo endelevu  visiwani Zanzibar kwa kuzingatia Ushirikishwaji, mazingira rafiki, rasilimali watu na vifaa kutaimarisha zaidi Uchumi wa Zanzibar kupitia Uchumi wa Buluu.

Imetolewa na kitengo Cha Habari (OMPR)

Leo tarehe 06.11.2023

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.