Habari za Punde

ZU waandaa jukwaa la siku ya Saikolojia

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Hassan Khamis Hafidh akizungumza na wadau wa saikojia wakati akifungua Jukwaa la siku ya saikolojia lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Zanzibar  ZU na kufanyika  Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-Wakil Kikwajuni Mjini Unguja.
Baadhi ya wadau wa Saikolojia wakifuatilia hafla ya Jukwaa la siku ya Saikolojia lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Zanzibar  ZU na kufanyika  Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-Wakil Kikwajuni Mjini Unguja
Msanii wa tungo za mashairi Kassim Yussuf  akisoma utenzi wenye maudhui ya umuhimu wa taaluma ya tiba ya saikolojia na Ushauari nasihi katika Jukwaa la siku ya Saikolojia lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Zanzibar  ZU na kufanyika  Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-Wakil Kikwajuni Mjini Unguja


Na Imani Mtumwa  Maelezo- Zanzibar                     12/11/2023

 

Wanasaikolojia wametakiwa kufanya uchunguzi  wakati wanapofanya kazi zao ili kuleta maendeleo katika jamii kwani taaluma hiyo inasababisha kupatikana ufumbuzi wa haraka

 

Wito huo umetolewa na Naibu waziri wa Afya Mhe Hassan Khamis Hafidh wakati akizindua  jukwaa la siku ya Saikolojia Ukumbi wa Idrisa Abdulwaki Kikwajuni Zanzibar

 

Aidha amefahamisha kuwa taaluma  hiyo ni muhimu kupatiwa Vijana kwani elimu ya Saikolojia inahitajika katika harakati mbali mbali za maendeleo

 

Hata hivyo amesema matibabu ya Saikolojia nimuhimu   kwa Wagonjwa wanaosumbuliwa na maradhi sugu kama vile maradhi ya moyo, saratani hivyo wagonjwa hao wanahitaji tiba ya Saikolojia ili kuweza kukubaliana na hali hiyo.

 

Nae Katibu mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Khamis Abdallah amewapongeza   Jumumuia ya Wanafunzi Saikolojia (ZUPCSA) Kwa kuandaa Jukwaa  hilo   linalosaidia kutoa Elimu kwa jamii.

pamoja na hayo katibu huyo liwaomba wadau wa Saikolojia kuunga mkono juhud za ZUPCSA za kuendeleza kufanya   Jukwaa hilo kila Mwaka.

 Akisoma  Risala kwaniaba ya ZUPCSA Mwekiti wa jumuia hiyo Ramadhan Muhammed amesema Taaluma hiyo bado ni mpya hivyo wanaendelea kutota Elimu kwa jamii kuweza kufahamu umuhimu wa Taauma hiyo.

  

Hata hivyo waliiomba Serekali kuanzisha chombo au bodi maalum   itakayosimamia wahitimu wa taaluma hiyo  kuweza kupatiwa leseni na kutambulika kama zilivyo taaluma nyengine nchini.

 

 

Jukwaa  la siku ya Saikolojia ni latatu kufanyika tangu kuanzishwa taluuma hiyo katika Chuo Kikuu cha Zanzibar ambapo Mwaka huu jukwaa hilo limebeba ujumbe “Afya ya Akili na Tiba ya Saikolojia ni haki kuu ya Binaaadamu.” 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.