Habari za Punde

Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe.Dkt.Jakaya Kikwete Aongoza Bodi ya Wakurugenzi wa GPE Kutembelea Skuli Zanzibar

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Makamu Mwenyekiti wake Susan Liautaud na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti, na ujumbe wao wakiwa Skuli ya msingi ya Kisiwandui mjini Magharibi.

 

Na Mwandishi Maalumu.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Makamu Mwenyekiti wake Susan Liautaud na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti, leo wametembelea na kukagua skuli zinazopata ufadhili na shirika hilo.

Katika ziara ya leo ujumbe huo mzito wa GPE ulitembelea na kukagua skuli ya Maandalizi ya ya Kikaangoni  pamoja na Skuli ya msingi ya Kisiwandui, ukiwa umeongozana na wenyeji wao Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe Lela Mohamed Mussa,  na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi,  Mhe Suzan Peter Kunambi.

Huo ni mwendelezo wa ziara ya viongozi na wajumbe wa bodi ya GPE kutembelea miradi mbalimbali yya bara na visiwani kabla Dkt. Kikwete, akiwa mwenyekiti wa Bodi hio ataongoza vikao vya Shirika hilo hapa Zanzibar kuanzia leo  4 hadi 6 Disemba, hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kwa Shirika hilo la kimataifa kufanya vikao vyake vya bodi barani Afrika na nje ya Marekani na Ulaya.

GPE iliyoanzishwa mwaka wa 2002, ni Shirika lililoundwa na mataifa Tajiri duniani ya G& na linasimamiwa na Benki ya Dunia, kufadhili maendeleo ya  elimu katika nchi zinazoendelea.

Majukumu ya GPE ni pamoja na  kusaidia serikali za nchi zinazoendelea kufanya mabadiliko ya kimfumo na kuoanisha rasilimali na ufadhili ili kutoa elimu bora kwa watoto Wote, kuinua viwango vya kujifunza na kukabiliana na changamoto mpya nchini.

Kwa mujibu wa Dkt. Kikwete, ambaye ni Mwafrika wa kwanza kuongoza GPE, shirika hilo hadi sasa limeishaipatia Tanzania jumla ya  Dola za Kimarekani Milioni 332 (takriban shilingi 834,980,332,000.00) ili kusaidia sekta ya elimu bara na visiwani.

Majuzi GPE imetiliana saini na Serikali ya makubaliano ya kutoa dola za Kimarekani milioni 85 (takriban shilingi 213, 775, 085, 000.0)    kwa ajili ya kusaidia mafunzo ya  walimu nchini.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Makamu Mwenyekiti wake Susan Liautaud na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti, wakilakiwa kwa  burudani waliopowasili skuli ya Maandalizi ya Awali  ya Kikaangoni Wilaya ya Magharibi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Makamu Mwenyekiti wake Bi Susan Liautaud (mwenye barakoa) na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali  Mhe Lela Mohamed Mussa (kushoto kwa Dkt Kikwete)  wakiangalia wanafunzi  katika  darasa la skuli ya Maandalizi ya Awali  ya Kikaangoni Wilaya ya Magharibi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na  na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti, wakifurahia mchoro wa mwanafunzi katika skuli ya Maandalizi ya Awali ya Kikaangoni Wilaya ya Maagharibi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Makamu Mwenyekiti wake Bi Susan Liautaud (mwenye barakoa) wakiwa na mototo wa mmoja wa wazazi wa watoto wanaosoma skuli ya Maandalizi ya Awali  ya Kikaangoni Wilaya ya Maagharibi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Makamu Mwenyekiti wake Susan Liautaud na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bibi Laura Frigenti, na ujumbe wao wakiwa Skuli ya msingi ya Kisiwandui mjini Magharibi.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.