Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango
akiagana na Mbunge wa Monduli Mhe. Fredy Lowassa ambaye ni Mtoto wa Waziri Mkuu
Mstaafu marehemu Edward Lowassa mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo na
kuwafariji wafiwa katika makazi ya familia Masaki Jijini Dar es salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiweka Saini katika kitabu cha maombolezo
kufuatia kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu
Edward Lowassa wakati alipofika katika Makazi ya Familia Masaki Jijini Dar es
salaam tarehe 11 Februari 2024. Kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye
Mpango.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimfariji mjane wa Waziri Mkuu Mstaafu marehemu Edward Lowassa
,Mama Regina Lowassa mara baada ya kuwasili nyumbani kwa familia hiyo Masaki
Jijini Dar es salaam.
Mke wa Makamu wa Rais
Mama Mbonimpaye Mpango akimfariji mjane wa Waziri Mkuu Mstaafu marehemu Edward
Lowassa , Mama Regina Lowassa mara baada ya kuwasili nyumbani kwa familia hiyo
Masaki Jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwafariji waombolezaji mbalimbali wakati
alipofika nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu marehemu Edward Lowassa Masaki
Jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment