Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Asaini Kitabu cha Maombelezi Kufuatia Kifo chas Waziri Mkuu Mstaafu Marehemu Edward Lowassa

 







RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema amewahi kufanya kazi na Hayati Edward Lowassa kwa vipindi tofauti katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya awamu ya tatu na awamu ya nne. 

Amesema taarifa ya msiba huu ameipokea kwa masikitiko makubwa, pia anatoa pole kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wananchi wote kwa ujumla.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipofika nyumbani kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Hayati Edward Lowassa, akiwa na Mama Mariam Mwinyi, kwa lengo la kuwafariji wanafamilia wa marehemu akiwemo Mama Regina Lowassa, Masaki, Jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Februari 2024

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.