Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mhe Majaliwa Ziarani Wulaya ya Ruangwa

Waziri Mkuu na Mbunge wa Ruangwa Kassim Majaliwa akiwasalimia wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia alipotembelea Shule hiyo iliyopo Ruangwa mkoani Lindi.

Waziri Mkuu na Mbunge wa Ruangwa Kassim Majaliwa akiwasalimia wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia alipotembelea Shule hiyo iliyopo Ruangwa mkoani Lindi.

Waziri Mkuu na Mbunge wa Ruangwa Kassim Majaliwa akimuangalia Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Lucas Malia Greater david akifanya majaribio ya kuwasha umeme kwa kutumia Sakiti kupitia Kompyuta, wakati alipotembelea shule hiyo. 
Waziri Mkuu na Mbunge wa Ruangwa Kassim Majaliwa akikagua maabara ya kompyuta alipotembelea Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia iliyopo Ruangwa mkoani Lindi, 
Waziri Mkuu na Mbunge wa Ruangwa Kassim Majaliwa akizungumza na wazazi na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia alipotembelea Shule hiyo iliyopo Ruangwa mkoani Lindi, leo Februari 22, 2024
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuhakikisha Shule zote nchini zinakuwa na mifumo bora ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kurahisisha ujifunzaji na ufundishaji kwenye ngazi zote za elimu.

 

Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Februari 22, 2024) wakati alipotembelea na kukagua miundombinu ya TEHAMA iliyowekwa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia, Ruangwa Mkoani Lindi. 

 

Akizungumza na wazazi na wanafunzi wa Shule hiyo Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa kwa kuwezesha kufunga mifumo ya TEHAMA katika shule hiyo.

 

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa, amesema Shule hiyo ya Lucas Malia itakuwa kitovu cha ufundishaji kupitia mifumo ya TEHAMA kwa shule za Sekondari Wilayani Ruangwa. 

 

Katika hatua nyingine Mheshimiwa Majaliwa amesema wana Ruangwa wana kila sababu ya kumshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na manufaa ambayo Wilaya hiyo imepata kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali.

 

"Wana-Ruangwa niwakati wetu wa kujivunia uwepo wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, jukumu lenu ni lilelile la kuniunga mimi mkono nifanye kazi, na kumuunga mkono Rais wetu Dkt. Samia afanye kazi yake vizuri, lazima mjivunie, mumuombee, mumsemee, mumtetee na kumuunga mkono katika kila jambo lake”

(mwisho)

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

ALHAMISI, FEBRUARI 22, 2023.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.