Habari za Punde

Waziri wa Fedha Mhe.Dkt. Nchemba Ateta na Balozi wa Denmark Nchini Tanzania --Mema Yaja

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Denmark hapa nchini, Mhe. Mette Dissing-Spandet, ambapo ameishukuru nchi hiyo kwa kuchangia maendeleo ya Tanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii pamoja na ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Morogoro hadi Makutupora mkoani Singida. Mkutano huo umefanyika Katika Ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, Jijini Dodoma. 

(Picha na KItengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Fedha-Dodoma)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.