Habari za Punde

Bank of Africa yafuturisha wateja wake Zanzibar

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya BOA Ndg.Wasia Mushi akizungumza na kutowa shukrani kwa Wananchi na Wateja wao na kueleza huduma zimazotolewa na benki hiyo, wakati wa hafla ya Iftar iliyoandaliwa kwa ajili yao katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar leo 7-4-2024.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Ali Abdulgulam Hussein akizungumza katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Bank of Africa kwa Watejao wao wa Zanzibar iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar leo 7-4-2024.  

Bank of Africa Tanzania (BOA) imeeleza dhamira yake ya  kuimarisha huduma zake zake zaidi kwendana na matakwa  ya wateja sambamba na kuunga mkono jitihada za Serikali za kuwawezesha wanachi  ili waweze kujipatia maendeleo sambamba na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.

Akiongea katika Iftar iliyoandaliwa na Benki hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Wasia Mushi, alisema benki hiyo itaboresha na kuendelea kukuza huduma zake za kibenki ikiwamo huduma za uwakala , simu na mifumo yote ya matumizi ya teknolojia (Tehama) katika jitihada za kukuza biashara na kuchochea ukuaji wa uchumi na kuwezesha makundi ya biashara ndogo na biashara za kati.

“benki yetu inatoa ahadi kuendelea kutoa huduma bora na uwajibikaji wa hali juu katika kuhakikisha ustawi wa wateja wetu na kuchochea maendeleo uchumi katika sekta mbalimbali hapa nchini,” aliongeza Bw Mushi

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema kuwa ni heshima kwa uongozi wa Benki kuandaa Iftar kwa wateja wa benki hiyo, pamoja na kukuza hisia za jumuiya kati ya imani mbalimbali.

Alisisitiza zaidi umuhimu wa kushiriki pamoja kupata Iftar katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na umuhimu wa kuishi pamoja kidini na kuheshimiana kwa ajili ya kudumisha amani, maelewano na ustawi wa jamii.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ali Abdulgulam Hussein aliipongeza Benki ya Afrika Tanzania kwa kuandaa Iftar, na kwa jitihada inazofanya kushirikiana na Serikali katika kuwaletea Wananchi maendeleo.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Ali Abdulgulam Hussein akiwa na wageni waalikwa katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Bank of Africa kwa Wateja wao wa Zanzibar  iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar leo 7-4-2024.  
Wateja wa Bank of Africa wakishiriki katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Benki hiyo katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar leo 7-4-2024.
Wateja wa Bank of Africa wakishiriki katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Benki hiyo katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar leo 7-4-2024.

Bank of Africa Tanzania (BOA) imeeleza dhamira yake ya  kuimarisha huduma zake zake zaidi kwendana na matakwa  ya wateja sambamba na kuunga mkono jitihada za Serikali za kuwawezesha wanachi  ili waweze kujipatia maendeleo sambamba na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.

Akiongea katika Iftar iliyoandaliwa na Benki hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Wasia Mushi, alisema benki hiyo itaboresha na kuendelea kukuza huduma zake za kibenki ikiwamo huduma za uwakala , simu na mifumo yote ya matumizi ya teknolojia (Tehama) katika jitihada za kukuza biashara na kuchochea ukuaji wa uchumi na kuwezesha makundi ya biashara ndogo na biashara za kati.

“benki yetu inatoa ahadi kuendelea kutoa huduma bora na uwajibikaji wa hali juu katika kuhakikisha ustawi wa wateja wetu na kuchochea maendeleo uchumi katika sekta mbalimbali hapa nchini,” aliongeza Bw Mushi

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema kuwa ni heshima kwa uongozi wa Benki kuandaa Iftar kwa wateja wa benki hiyo, pamoja na kukuza hisia za jumuiya kati ya imani mbalimbali.

Alisisitiza zaidi umuhimu wa kushiriki pamoja kupata Iftar katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na umuhimu wa kuishi pamoja kidini na kuheshimiana kwa ajili ya kudumisha amani, maelewano na ustawi wa jamii.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ali Abdulgulam Hussein aliipongeza Benki ya Afrika Tanzania kwa kuandaa Iftar, na kwa jitihada inazofanya kushirikiana na Serikali katika kuwaletea Wananchi maendeleo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.