Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Atembelea Hospitali ya Mnazi Mmoja na ya Wilaya ya Magharibi B Unguja leo

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akisalimiana na wagonjwa waliolazwa katika wodi ya mifupa katika hospital ya Rufaa ya Mnazi Mmoja wakati alipofanya ziara ya  kutetembelea na kukagua utowaji wa huduma katika hospitali hiyo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla ametoa agizo kwa uongozi wa Kampuni ya Lancet kuhakisha ndani ya mwezi mmoja kitengo cha wagonjwa walio katika uangalizi maalum (ICU) katika hospitali ya Wilaya ya Magharibi “B” Mwanakwerekwe Ijitimai kinatoa huduma ili kuondoa usumbufu wa ongezeko la wagonjwa katika hospital ya Rufaa ya Mnazi Mmoja.

Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea na 

kukagua maendeleo ya utowaji na upatikanaji wa huduma za 

Afya kwa wananchi katika hospital ya Wilaya ya Magharibi 

“B” Mwanakwerekwe Ijitimai na Hospital ya Taifa ya Rufaa ya 

Mnazi Mmoja Mkoa wa Mjini Magharibi.

Amesema kuwa Kampuni ya Lancet ina wajibu wa 

kuhakikisha huduma zote muhimu zinapatika kwa ubora na 

haraka kwa wagonjwa wanaofika katika hospitali zote za 

Wilaya ili kuondosha msongamano wa wagonjwa katika 

hospital za Rufaa ya Mnazi Mmoja.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali ya 

Awamu ya Nane imelipa kipaombele suala la kuboresha 

miundombinu ya Afya ili kuzidi kutoa huduma bora za 

kitabibu kwa Wananchi hivyo wananchi wanapaswa kuunga 

mkono juhudi zinazochukuliwa na viongozi katika kuwaletea 

maendeleo ikiwemo upatikanaji wa huduma bora za Afya.

Mhe. Hemed amewasisitiza madaktari kudumisha nidhamu 

katika kazi kwa kufuata miiko, miongozo na maadili ya kazi 

zao na kuachana na tabia ya kuwatolea lugha chafu wagonjwa 

hasa wahuduma za Dharura  ili kuendelea kuilinda heshima 

ya  wananchi ambapo Serikali haitamvumilia mtu yoyote 

atakae kwenda kinyume na maadili ya kazi na itamchukulia 

hatua za kisheria na kinidhamu kwa haraka .

Aidha Makamu wa Pili wa Rais  amezitaka kampuni ya  

Lancet na NSK zinazotoa huduma katika hospital za Wilaya na 

Hospital ya Rufaa ya Mnazi Mmoja kuhakikisha changamoto 

zote za vifaa, wataalamu na kiutendaji zinapatiwa ufumbuzi 

kwa haraka ili kupunguza malalamiko kwa wananchi ambao 

wameipa Imani Serikali yao ya kiwatumikia na kuwaletea 

maendeleo.

Sambamba na hayo amewasisitiza wananchi kuendelea 

kuzitumia Hospitali za Wilaya katika kutafuta matibabu 

ambazo zinatoa huduma zote za kitabibu ili kupunguza wingi 

wa wagonjwa katika hospitali za Rufaa.

Makamu wa Pili wa Rais amesema kuwa Serikali kuu 

itahakikisha inatatua chamgamoto zote zinazoikabili Sekata 

ya Afya zitapatiwa ufumbuzi wa haraka ili kuendelea kutoa 

huduma bora na stahiki kwa wananchi bila ya ubaguzi wa aina 

yoyote.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital ya Rufaa 

ya Mnazi Mmoja Dkt. Muhiddin Abdi Mahmoud amesema 

katika kupunguza changamoto ya wataalamu katika 

Hospitali za Wilaya na Rufaa Wizara ya Afya imeamua 

kusomesha wafanyakazi wake kwa kuwalazimisha kusomea 

zile kada ambazo zina upungufu wa madaktari ili kuweza 

kutoa huduma zilizo bora na kwa wakati.

Amesema kuwa Wizara ya Afya imepanga kuandaa utaratibu 

wa kuwashauri na kuwashawishi wanafunzi wanaojiunga na 

vyuo vikuu kusomea kozi ambazo zina uhaba wa wataalamu   

ikiwemo ICU, Ganzi na Usingizi pamoja na Huduma za 

dharura ili kuweza kulisaidia Taifa kupata wataalamu wazawa.

Kwa upande wao wananchi waliofika hospitalini hapo kwa 

ajili ya kupatiwa matibabu wameishukuru Serikali ya 

Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwajengea hospitali za Wilaya na 

kuwasogezea huduma za matibabu karibu na makazi yao 

zinazotoa huduma bora na kwa wakati sambamba na 

kuwashukuru Madaktari kwa huduma bora wanazowapatia 

wagonjwa wanaofika hospitalini hapo.

uhidin UHIDDIN ABDI MAHMOUD 

amesema katika kupunguza changamoto ya wataalamu katika 

Hospitali za Wilaya na Rufaa Wizara ya Afya imeamua 

kusomesha wafanyakazi wake kwa kuwalazimisha kusomea 

zile kada ambazo zina upungufu wa madaktari ili kuweza 

kutoa huduma zilizo bora na kwa wakati.

Amesema kuwa Wizara ya Afya imepanga kuandaa utaratibu 

wa kuwashauri na kuwashawishi wanafunzi wanaojiunga na 

vyuo vikuu kusomea kozi ambazo zina uhaba wa wataalamu   

ikiwemo ICU, Ganzi na Usingizi pamoja na Huduma za 

dharura ili kuweza kulisaidia Taifa kupata wataalamu wazawa.

Kwa upande wao wananchi waliofika hospitalini hapo kwa 

ajili ya kupatiwa matibabu wameishukuru Serikali ya 

Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwajengea hospitali za Wilaya na 

kuwasogezea huduma za matibabu karibu na makazi yao 

zinazotoa huduma bora na kwa wakati sambamba na 

kuwashukuru Madaktari kwa huduma bora wanazowapatia 

wagonjwa wanaofika hospitalini hapo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.