Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Ameweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Afisi ya Uhamiaji ya Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Ikiwa Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya vMuungano wa Tanzania

MEONEKANO wa Jengo jipya la Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Mjini Magharibi Jijini Zanzibar, linalojengwa katika eneo la Mazizini Wilaya ya Mgharibi “B” Unguja lililowekwa Jiwe la Msingi la ujenzi huo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, ikiwa ni Shamrashamra za Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania, hafla hiyo iliyofanyika leo 19-4-2024.
WASANII wa Kikundi cha Mafunzo Zanzibar wakitowa burudani ya Ngoma ya Kibati wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Afisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja linalojengwa katika eneo la Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, ikiwa ni Shamrashamra ya Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania, hafla hiyo iliyofanyika leo 19-4-2024.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Serikali  alipowasili katika viwanja vya ujenzi wa jengo jipya la Idara ya Uhamiaji la Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, linalojengwa katika eneo la Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar, ikiwa ni Shamrashamra za Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania, hafla hiyo iliyofanyika leo 19-4-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein  Ali Mwinyi akimsikiliza Mshauri Elekezi kutoka Wakala wa Majengo Zanzibar Mhandisi Hassan Haji Mrisho, akitowa maelezo ya Kitaalamu ya ujenzi wa Jengo la Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, linalojenwa katika eneo la Mazizini Unguja, ikiwa ni Shamrashamra za Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Masauni,na (kulia kwa Rais) Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt.Anna Peter Makalala hafla hiyo iliyofanyika leo 19-4-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Mhe. Hamad Masauni (kushoto) kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Idara ya Uhamiaji la Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Zanzibar, ikiwa ni shamrashamra za Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania,hafla hiyo iliyofanyika leo 19-4-2024






RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la ujenzi wa Afisi ya Uhamiahi ya Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Jijini Zanzibar, inayojengwa katika eneo la Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja, ikiwa ni Shamrashamra za Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania, hafla hiyo iliyofanyika leo 19-4-2024

WAFANYAKAZI Wastaafu wa Idara ya Uhamiaji Tanzania wakifuatila hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Afisi ya Uhamiaji ya Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya ujenzi wa jengo hilo Mazizini Wilaya ya Magharibi ”B” Unguja Jijini Zanzibar, ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania iliyofanyika leo 19-4-2024.

BAADHI ya Viongozi wa Vyama vya Siasa Zanzibar wakifuatilia hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa jengo la Afisi ya Idara ya Uhamiaji la Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, linalojengwa katika eneo la Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania, hafla hiyo iliyofanyika leo 19-4-2024

VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Afisi ya Uhamajia Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, hafla hiyo iliyofanyika leo 19-4-2024 ikiwa ni Shamrashamra za sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mhandisi Hamad Masouni na Viongozi wengine baada ya kumalizika kwa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Afisi ya Uhamiaji ya Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Jijini Zanzibar, iliyofanyika leo 19-4-2024 ikiwa ni Shamrashamra za sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.