Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji
wake Rais wa Uturuki Mhe.
Recep Tayyip Erdogan wakati wakiangalia album ya picha za matukio
ya Ziara Rasmi aliyoifanya katika
Ikulu ya Kulliye Ankara nchini Uturuki
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na
Waandishi wa Habari wakati wa Ziara yake Rasmi katika Ikulu Kulliye Ankara nchini
Uturuki
Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan
akizungumza na Waandishi
wa Habari kuhusu Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan katika Ikulu Kulliye
Ankara nchini Uturuki
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekea kuweka shada
la maua katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Uturuki Hayati Mustafa Kemal Atatürk
katika makumbusho ya Anitkabir, Atatürk's Jijini Ankara nchini Uturuki
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Heshima
mbele ya kaburi la Rais wa Kwanza wa Uturuki Hayati Mustafa Kemal Atatürk
katika makumbusho ya Anitkabir, Atatürk's Jijini Ankara nchini Uturuki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la Rais wa Kwanza wa Uturuki Hayati Mustafa Kemal Atatürk katika makumbusho ya Anitkabir, Atatürk's Jijini Ankara nchini Uturuki
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan wakati wakishuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba na kwa upande wa Uturuki Rais wa Baraza la Elimu Profesa Dkt. Erol Ozvar wakitia saini Makubaliano ya Ushirikiano katika Nyanja ya Elimu ya Juu baina ya Tanzania na Uturuki.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa
Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na Mwenyeji wake Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan katika Ikulu
ya Kulliye Ankara nchini Uturuki
Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip Erdogan
akiongoza ujumbe wa Nchi yake kwenye mazungumzo Rasmi na ujumbe wa Tanzania
ulioongozwa na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Ikulu ya Kulliye Ankara
nchini Uturuki
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip
Erdogan wakati wakishuhudia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa
Zanzibar Lela Muhamed Mussa pamoja na Rais wa Baraza la Utalii la Jamhuri ya
Uturuki Abdullah
Eren
wakisaini hati za makubaliano kwa ajili ya kuanzisha ufadhili kwa wanafunzi
wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Uturuki wanaohitimu katika
Elimu ya Juu
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Uturuki Mhe. Recep Tayyip
Erdogan wakati wa utiaji saini Hati za makubaliano kati
ya Ofisi ya Rais Uwekezaji ya Jamhuri ya Uturuki iliyowakilishwa na Zeynel Kılınç, Makamu wa Rais wa Ofisi
ya Rais Uwekezaji ya Jamhuri ya Uturuki na kwa upande wa Tanzania iliwakilishwa
na Mkurugenzi Mkuu wa
Kituo cha Uwekezaji TIC Bw. Gilead Teri.18-4-2024.
No comments:
Post a Comment