Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Afungua Makumbusho ya Amani na Viumbe Hai Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akikata Utepe kuashiria Ufunguzi wa Makumbusho ya Amani na Viumbe Hai katika Eneo la Mnazi Mmoja  jijini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Kale Bi. Maryam Mansab wakati wa Ufunguzi wa Makumbusho ya Amani na Viumbe Hai katika Eneo la Mnazi Mmoja jijini Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  MHE. HEMED SULEIMAN ABDULLA amesema Makumbusho ya Amani na Viumbe Hai yatasaidia katika kukuza Sekta ya Utalii na kukuza uchumi wa nchi kwa vile ni kivutio kikubwa cha wageni walio wengi wanaoitembelea Zanzibar.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Makumbusho ya 

Amani na Viumbe hai yaliyopo Mnazi Mmoja jijini Zanzibar.

 

Amesema Serikali imejipanga kufanya ukarabati katika maeneo yote ya kihistoria ikiwemo eneo la kihistoria la Fufuni Pemba,  Msikiti wa Kihistoria wa kichokochwe Pemba, eneo la kihistoria la Maruhubi pamoja na Mahamamu ya Forodhani, Kijichi, Hamamni na Kizimkazi Unguja kwa lengo la kukuza sekata ya utalii pamoja kuengeza pato la nchi.


Mhe. Hemed  amefahamisha kuwa Serikali kupitia Wizara ya 

Utalii na Mambo ya Kale itaendelea kuyaendeleza maeneo ya 

kihistoria kwa kuzungusha ukuta, Uwekaji wa vitu vya kale, 

kuyajenga ili kurudisha uasili wake  sambamba na kuimarisha 

majengo ya utoaji wa huduma kama vile vyoo, migahawa na 

maduka.


Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar  amesema  kwa kutambua na kuthamini umuhimu mkubwa wa Makumbusho, Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya Mwaka 2020-2025 imechukua hatua ya kuweka mazingira mazuri katika maeneo ya Makumbusho kwa kutunga Sheria ya Uhifadhi wa mambo ya kale No.11 ya mwaka 2022 inayosimamia kutunza, kuhifadhi na kuendeleza Makumbusho ya Mambo ya Kale.


Aidha  Mhe. Hemed amewataka wafanyakazi wa Makumbusho ya Amani na viumbe hai pamoja na Makumbusho mengine kuendelea kuyaimarisha na kuyatunza ili yaendelee kuwa kivutio cha wageni wengi zaidi wa ndani na nje ya nchi.

Sambamba na hayo, Mhe. Hemed ametoa wito kwa jamii 

kutokuyavamia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya 

Makumbusho ya historia na badala yake waendelee 

kushirikiana na Serikali katika kuyalinda na kuyaimarisha ili 

kuendelea kuongeza vivutio vya utalii Zanzibar sambamba na 

kuwataka kujenga tabia ya kutembelea maeneo ya 

Makumbushoya kihistoria ili kujifunza mambo mbali mbali ya 

kihistoria  katika nchi yetu.

 

Nae Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar MHE. MUDRIK RAMADHAN SORAGA amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha   inahuwisha Sekta ya Utalii na Mambo ya Kale kwa kuyafungua Makumbusho  yote ambayo yalikuwa hayafanyi kazi ndani ya Zanzibar.

 

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Utalii imejipanga katika kuyajenga na kuyafanyia ukarabati maeneo ya Kihistoria na maeneo mengine ambayo ni vivutio vya Watalii ili kurejea katika hadhi yake jambo ambalo litapelekea kukuza  pato la mtu mmoja mmoja na la Taifa kwa ujumla.

 

Akisoma taarifa ya Kitaalamu juu ya Uzinduzi wa Makumbusho ya Amani na Viumbe Hai, Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Dkt. ABOUD SULEIMAN JUMBE  amesema  kupitia mradi wa kuhifadhi na kuendeleza maeneo ya urithi Serikali imeamua kuyafanyia ukarabati na kuimarisha maonesho ya  Makumbusho ili kutarejesha katika haiba yake hasa kwa vile baadhi yao ni urithi muhimu wa Kitaifa na Kimataifa.

 

Dkt. Jumbe amesema kuwa Makumbusho ya Amani na Viumbe Hai yana umuhimu mkubwa katika uimarishaji wa Elimu na Utafiti, kuchangia uimarishaji wa Utalii wa ndani na nje katika kukuza uchumi wa nchi pamoja na kuhakikisha uhifadhi wa urithi wa kihistoria na kiutamaduni kwa vizazi vijavyo.

 

Zaidi ya shilingi Bilioni saba(7) zimetumika katika ukarabati wa Makumbusho hayo kwa kuzifanyia ukarabati kuta na sakafu ndani na nje, ujenzi wa mabanda ya viumbe haipamoja  na urejeshaji wa viumbe hai, ukarabati wa maabara pamoja na uwekaji wa vifaa vya teknolojia ya habari na mawasiliano ambavyo vitatumika katika kutoa elimu kwa wageni.

 

 Imetolewa kitengo cha Habari (OMPR)

Tarehe …29.05.2024

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.