Mwenyekiti wa Chama cha ACT- Wazalendo taifa Mhe. Othman
Masoud Othman, amesema kwamba chama hicho kinalenga kufikisha mawazo mbadala
kwa watanzania kwa dhamira ya kuunga nguvu za pamoja ili kusaidia kujenga nchi
kimaendeleo.
Mhe. Othman ambaye pia
ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ameyasema hayo alipokutana na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki
Kigoma Mhasham Joseph R. Mlola ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika Mkoani huo ikiwa ni maadhimisho ya chama hicho kutimia miaka kumi tangu kuanzishwa kwake .
Amesema kwamba kufanya hivyo ndio kutekeleza ipasavyo kazi ya
vyama vya siasa ambapo msingi wake mkuu ni kuumarisha kidemokrasia kwa kuwa chama
hicho hakiamini kwamba siasa ni mapambano
bali kinaamini ni namna bora ya kuweza kuwafikia watu na kuweza kushauriana
kwa mashirikiano juu ya namna bora ya kuleta mabadiliko .
Aidha amefahamisha kwamba msingi mwengine unaotumiwa na chama
hicho ni kuendeleza kukosoa kistaarabu
kwani kufanya hivyo hakuhitaji lugha ya kukirihisha bali ni kujenga usawishi kwa
watu na kuweza kukubalika.
Akizungunzia suala la
Katiba Mpya Mhe. Othman amesema kwamba jambo hilo ni muhimu kuwepo chombo cha
mawazo shirikishi ambalo ni Bunge lakini
Bunge lililopo sasa lina uwakilishi sahihi wa wananchi kutokana na kutokuwepo
uchaguzi huru na wa haki.
Hata hivyo, amesema kwamba Viongozi na Taasisi za dini
zinanafasi muhimu katika kujenga Imani
kwa wananchi na kuweza kufikia malengo yanayokusudiwa na taasisi za vyama vya
siasa.
Akizununzia suala la Serikali ya Umoja wa Kitaifa Mhe. Othman
amesema kwamba chama chake akioni furaha wala fahari ya kutananza kujitoa
lakini kinalazimika kufanya ivyo kutokana na mazingira ya kutokuwepo dhamira ya
kweli kama masarti ya kuingia kwenye serikali
hiyo jambo ambalo halikuwa rahisi.
Alisema kwamba Chama chake kipo tayari na kinakaribisha ushauri na maelekezo kutoka
kwa viongozi na taasisi za dini mbali mbali pale inapoonekana kwamba kuna mambo
hayaendi vyema kwa nia ya kuleta umoja kwenye ujenzi wa nchi.
Naye Askofu wa Jimbo Katoliki Kigoma Mhasham Josep R. Mlola
amekipongeza chama hico kwa kuweza
kujijenga na kusambaa nchi nzima katika kipindi kifupi cha miaka kumi tokea
kuanziswa kwake.
Amekitaka kuendelea kujitaidi kuwa sauti ya wasionasauti
kuwatetea watu wa Tanzania na kwamba ni muhimu kutumia mbinu ya mazungunzo
katika kufikia vyema maleno na matarajio ya wananchi kupitia majukwaa ya siasa.
Mhe. Othman yupo Mkoani Kigoma kuendelea na ziara yake ya
kuadimisa miaka kumi tokea kuanzishwa kwa chama hicho na anatarajiwa kumaliza ziara yake katika
Mkoa wa Tabora baadae wiki hii.
Imetolewa na ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo chake cha habari leo tarehe 07.05.04.
No comments:
Post a Comment