Habari za Punde

MJADALA WA UKARABATI MAJESTIC SCNEMA WAFUNGWA

Katibu Mtendaji wa Tume ya UNESCO ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Profesa Khamis Malebo akifunza warsha ya kujadili matumizi mazuri ya jego la sinema majestic baada ya kukamilika kwa matengenezo yake na kuwa kituo cha utalii huko hoteli ya Marumaru Shangani Mjini Unguja.

Baadhi ya wadau wa ukarabati jengo la majestic sinema wakijadili mikakati mzdhubuti itakayoweza kufanya ukarabati wa jengo hilo huko hoteli ya Marumaru Shangani Mjini Unguja.

PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR

Na Fauzi Mussa, Maelezo.

Katibu Mtendaji wa Tume ya UNESCO ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Profesa Khamis Malebo amesema ukarabati wa jengo la Majestic sinema utasaidia kuutangaza utamaduni wa  Nchi.

 Akifunga warsha  ya kujadili matumizi mazuri na uzinduzi wa ukarabati wa jengo hilo la kihistoria huko marumaru Shangani Wilaya ya Mjini amesema kukamilika kwa mradi huo kutaliwezesha jengo hilo kuendelea   kuonesha sinema mbalimbali ikiwemo filamu “Royal Tour” na “Serengeti haitangamia”  pamoja na maonesho ya kiutamaduni jambo ambalo litatoa fursa ya kuitangaza nchi  kwa watalii watakaofika katika jengo hilo na kuchangia  mapato ya Serikali kupitia sekta ya sanaa na utalii.

Alieleza kuwa  juhudi mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa ili kuhakikisha kila kitu katika jengo hilo kinabaki kuwa  salama na kuendelea kutumika kama  sehemu ya historia ndani ya  jengo hilo.

“jengo hili limebeba kumbukumbu za sinema mbalimbali za zamani ikiwemo mikanda na mashine zilizokuwa zikitumika kuoneshea sinema kwa wakati huo ambazo haziaptikani kwengine kokote hivyo kuendelea kutumika kwa jengo hilo kutawasaidia vijana wasasa kuona maendelelo ya teknolojia ya filamu ilipotoka hadi sasa.” Alifahamisha katibu Malebo

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Hifadhi  Mjimkongwe Zanzibar Ali Said Bakar amesema mradi huo utasaidia kurejesha baadhi ya vitu vilivyopotea ndani ya Mji huo  ikiwemo maonesho ya sinema na kuahidi kuendelea  kuyatunza na kuyaendeleza mambo ya urithi  yaliomo katika mji huo.

Aidha maefahamisha kuwa ukarabati huo hautaathiri muonekano wa jengo hilo na kuhakikisha linabakia katika muonekano wake wa asili na kuendelea kubakia kuwa jengo la kihistoria.

Alifahamisha kuwa jengo hilo mbali ya kuwa kituo cha utamaduni lakini pia litatoa fursa  kwa wajasiriamli wadogowadogo kuweza  kuuza biasharra zao ka wageni na wazawa pindi watakapofika kupata huduma maeneo hayo.

Sambamba na hayo amewataka wananchi na watumiaji  wa Mjimkongwe kuwa wastahmilivu katika kipindi chote cha ukarabati wa jengo hilo kwani lengo lake ni kuliimarisha na kuleta maslahi kwa jamii na Taifa kwa ujumla .

“changamoto mbalimbali zitajitokeza ikiwemo zogo, vumbi wakati wa ukarabati niwaombe tuwe wastahmilivu katika kipindi chote  cha kulikarabati jengo hili” alisema  mkurugenzi mamlaka ya hifadhi

Nae Sheha wa shehia ya Mnazimmoja Mohammed Juma Mugheir ameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuangalia   majengo mengine ndani ya Mjimkongwe yenye uwezekano wa kuwapatia wasanii wa utamaduni  kuweza kufanyia kazi zao kwani kuwakusanya wasanii  ndani ya Mji huo ambao ni kitovu cha Utalii kutatoa fursa kwa wasanii hao kuutangaza utamaduni wa Zanzibar kwa wageni wanaoingia nchini na kutembelea eneo hilo.

Pia Sheha huyo ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kukubali kulifanyiwa ukarabati kwa  jengo hilo na kuongezewa matumizi mbalimbali yakiwemo ya  kijamii.

Nao Wadau wanaotarajiwa kunufaika na uimarishwaji wa jengo la sinema majestic wakiwemo sauti za busara na Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar Ziff wamesema kuongezewa matumizi jengo hilo kutawapa fursa ya kutanua wigo wa kukuza utamaduni na Sanaa ya Zanibar.

Hata hivyo wamesema jengo hilo litawasaidia Wasanii wa Zanzibar kuweza Kukuza na kutangaza vipaji vyao sambamba na kuirithisha Sanaa ya kale kwa vizazi vya sasa.

Mtaalamu wa majengo ya kale Mwalim A. Mwalimu amesema ukarabati wa majestic sinema unahitaji takribani dola milioni  moja ambapo wadau mbalimbali wameanza kujitokeza  kusaidia ukarabati huo wakiwemo Serikali ya Japan na Saudia Arabia.

Amefahamisha kuwa wakati ukarabati huo ukiendelea  jumuiaya ya hifadhi imejipanga kuendelea kutafuta fedha kutoka kwa wadau wengine ili kukamilisha malengo waliojipangia.

MAELEZO YA PICHA

PICHA NO.01:- Katibu Mtendaji wa Tume ya UNESCO ya Jamuhuri ya Muun

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.