Rais Dk. Mwinyi ameyaeleza hayo Ikulu Zanzibar, alipozungumza na
Balozi mpya wa Brazil nchini Tanzania, Mhe. Gustavo Martins Nogueira na ujumbe wake wake aliofika
kujitambulisha.
Katika mazungumzo yao wamegusia kuendeleza uhusiano uliopo baina
ya Zanzibar na Brazil kwenye nyanja mbalimbali za miradi ya maendeleo ikiwemo sekta
ya Afya, miundombinu ya barabara, ujenzi wa uwanja wa ndege wa Pemba, kuimarisha
ushirikiano wa biashara, Utalii pamoja na fursa za uwekezaji kwenye sekta ya mafuta
na gesi Zanzibar.
Kuhusu sekta ya biashara, Rais Dk. Mwinyi alimueleza balozi huyo
kwamba Zanzibar haina eneo kubwa kwa kilimo badala yake imejikita zaidi kwenye
Sekta ya Utalii na Uchumi wa Buluu pia ni kutuo kikubwa cha biashara kwa watu
kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Dk. Mwinyi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanbar itadumisha
ushirikiano wake na Brazili hususan kwenye biashara ya sukari na mchele ili
kupungumza mfumko wa bei za bidhaa hizo nchini.
Alisema, Zanzibar
imejaaliwa baraka ya visiwa vizuri vyenye mvuto vya Unguja na Pemba vyenye ardhi
ya uwekezaji, hivyo alimueleza balozi huyo kuangalia fursa ya uwekezaji kwenye
sekta ya mafuta na gesi ambako serikali imeelekeza nguvu zake huko kuvutia
wawekezaji kwa eneo hilo.
Akizungumzia Sekta ya Afya Rais
Dk. Mwinyi aliemweleza Balozi huyo nia ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kuendeleza ushirikiano mzuri uliopo baina yake na Brazili pia kudumisha na kuendelea
kutoa ushirikiano kwa timu ya madaktari wa Brazil wanaokuja Zanzibar kwa nia ya
kuendeleza ushirikiano wao kwenye sekta ya Afya hasa kwa sekta ya Afya ya uzazi.
Kwa upande
wake, Balozi Nogueira amemueleza Rais Dk. Mwinyi ushirikiano
wa pande hizo mbili za diplomasia na kwamba Serikali ya Brazil itaelekeza nguvu
zake zaidi kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa kwenye eneo la afya ya
uzazi.
Kuhusu ushirikiano
wa biashara Balozi Nogueira pia alimweleza Rais Dk. Mwinyi
kwamba Brazili ni msalishaji mkubwa wa Sukari duniani hivyo aliitaka Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar kushirikiana zaidi kwenye eneo hilo kwa watu wa pande
mbili hizo kunufaika na biashara ya Sukari.
Akizungumzia
sekta ya Miundombinu ikiwemo ya barabara na mawasiliano Balozi Nogueira pia alimuhakikishia Rais Dk. Mwinyi kuwa Brazil inaendeleza ushirikiano wake
na Tanzania hususan Zanzibar kwa kuangalia uwekezaji na kuimarisha uwanja wa
ndege wa Pemba ili kutoa fursa zaidi kwa sekta ya Utalii Zanbar kuimarika
maradufu.
Uhusiano wa Diplomasia
baina ya Tanzania na Brazil ulianza tangu mwaka 1970 na mwaka 1979 Brazili
yenye mji mkuu wake Brasilia kwa mara ya kwanza ilifungua ubalozi wake Dar es
Salaam, Tanzania, baadae mwaka 1991
iliufunga kutokana na changamoto za gharama za uendeshaji lakini mwezi Machi mwaka 2005 Brazili
iliufungua tena Ubalozi wake wa Dar es Salaam hadi sasa.
Aidha, Tanzania
nayo ilifungua ubalozi wake kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Brasilia mwaka 2007
na mwaka 2010 rais wa kwanza wa Brazil kuitembelea Tanzania alikua Rais wa 39
wa nchi hiyo, Luiz Inacio Lula da Silva ambae aliliongoza taifa hilo kutoka
mwaka 2003 hadi 2011.
IDARA YA MAWASILINO, IKULU ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment