Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Mwinyi Amewajulia Hali Wajane wa Waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Mjukuu wa Mwanamapinduzi Marehemu Hafidh Suleiman. Lukman Iddi Hafidh Suleiman, alipofika nyumbani kwa marehemu Kilimani Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 3-5-2024, kwa ajili ya kumjulia hali kuwasalimia na (kushoto kwa Rais) Mjane wa Marehemu Bi.Mtumwa Hussein Farahan
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Husseinn Ali Mwinyi akizungumza na kumsalimia Mjane wa Marehemu Mwanamapinduzi Hafidh Suleiman. Bi.Mtumwa Hussein Farahan, alipofika nyumbani kwa marehemu Kilimani Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 3-5-2024,kwa ajili ya kuwasalimia na kuwajulia hali familia.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kumjulia hali Mjane wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Hayati Alhajj Aboud Jumbe Mwinyi. Mama Fatma Mohamed Hassan (kushoto kwa Rais) alipofika nyumbani kwake Mombasa kwa Mchina Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 3-5-2024, kwa ajili ya kumsalimia na kujumlia hali yake.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsalimia Mtoto Imran Adim Salum, baada ya kumaliza kumsalimia Mjane wa Marehemu Rais Mstaafu wa Zanzibar Hayati Alhajj Aboud Jumbe Mwinyi, Mama Fatma Mohamed Hassan (kulia kwa Rais) alipofika nyumbani kwake Mombasa kwa Mchina leo 3-5-2024.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.