RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Balozi
wa Norway Nchini Tanzania Mhe.Tone Tinnes, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa
mazungumzo na kujitambulisha, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa
Ikulu Zanzibar leo 30-5-2024.
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameyasema
hayo Ikulu Zanzibar alipozungumza na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe.
Tone Tinnes aliyekuja kujitambulisha.
Kwenye
mazungumzo yao, wamegusia maeneo makuu manne ya ushirikiano uliopo baina pande
mbili hizo za diplomasia ikiwemo Sekta ya Umeme, Mafuta na Gesi, Afya na
Mazingira.
Kuhusu
umeme Rais Dk. Mwinyi alimueleza Balozi, Tinnes kuangalia uwezekano wa kuongeza
Ushirikiano uliopo baina ya Norway na Tanzania ikiwemo Zanzibar hasa kusambaza
umeme vijijini ili kuviendeleza vijiji hivyo.
Akizungumzia
sekta ya Mafuta na Gesi, Rais Dk. Mwinyi ameikaribisha Norway kuangalia fursa
za uwekezaji kwenye maeneo hayo.
Aidha, Rais
Dk. Mwinyi alimueleza Balozi Tinnes kuongeza ushirikiano kwenye sekta ya Afya
kupitia hospitali ya rufaa ya Mnazi Mmoja kwa wataalamu wa magonjwa ya moyo.
Akigusia
suala za Mazingira Rais Dk. Mwinyi alieleza Zanzibar na Norway zimekua na
ushirikinao mzuri kwenye maeneo hayo, sambamba na kuwawezesha na kuwaendeleza
wanawake wa Zanzibar.
Dk. Mwinyi
pia alimueleza Balozi huyo, kuangalia uwezakano wa kuwaendeleza wakulima wa
mwani wa Zanzibar kupitia sekta ya Uchumi wa Buluu.
Alisema,
Uchumi wa Buluu ni Sera kuu ya Zanzibar ya kukuza Uchumi wake ikifuatiwa na Utalii
unaochangia asilimia 30 ya pato la taifa.
Naye,
Balozi Tinnes alimuhakikishia Rais Dk. Mwinyi ushirikiano mzuri uliopo baina ya
Ubalozi huo na Shirika la Umeme, Zanzibar (ZECO) kupitia miradi mbalimbali ya
kimkakati ya kukuza huduma za umeme kwa visiwa vya Zanzibar.
Balozi
Tinnes alisema, ZECO na Ubalozi wa Norway nchini umefikia mazungumzo mazuri
kwenye kuimarisha ushirikiano wao kupitia miradi mbalimbali ya Shirika hilo.
Kuhusu
Sekta ya Afya, Balozi Tinnes alimueleza Rais Dk. Mwinyi ushirikino uliopo baina
ya hospitali ya Mnazi Mmoja na Hospitali kuu ya Norway kuwa pande mbili hizo
zinashirikiana kubadilishana uzoefu na kusaidiana wataalamu kwa maeneo tofauti.
Balozi
Tinnes pia alisifu ushirikiano mzuri uliopo baina ya Taasisi za kodi za
Tanzania ikiwemo Mamlaka ya Mapato Zanzibar, (ZRA) na taasisi ya kodi ya Norway,
alisema Tanzania na Norway zinashirikiano kwa kubadilisha uzoefu na utaalamu wa
maeneo hayo.
Pia Balozi
huyo, alipongeza hatua kubwa ya Maendeleo iliyofikiwa na Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar pamoja na kupongeza miaka 60 ya ushirikiano wa diplomasia uliopo
baina ya Tanzania na Norway uliotengeneza historia muhimu kwa jamii za pande
zote mbili za ushirikiano kiuchumi na jamii.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment