Habari za Punde

Wanafunzi Wametakiwa Kujiepusha na Vishawishi vya Mafataki Wanaotaka Kukatisha Ndoto ya safari Yao

Kaimu Kamanda Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gallus Hyera akizungumza na Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Bupigu, kujiepusha na Vishawishi vya mafataki. 

Na Issa Mwadangala

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bupigu iliyopo Wilaya ya Ileje mkoani Songwe wametakiwa kujiepusha na vishawishi vya mafataki wanaotaka kukatisha ndoto ya safari ya masomo yao.

Hayo yalisemwa Aprili 30, 2024 na Kaimu Kamanda Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gallus Hyera alipokuwa akitoa elimu juu ya madhara ya mimba za utotoni na ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa Shule hiyo.

Kamanda Hyera alisema “Jukumu la ulinzi wa wanafunzi na watoto ni letu sote hivyo basi kila mmoja anapaswa kushirikiana na Jeshi la Polisi kupinga ukatili ili ujumbe ufike kwa wepesi kwa jamii jambo ambalo litapelekea kupunguza ukatili katika mkoa huo”.

Kamanda Hyera alitoa wito kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya ukatili na uhalifu kuacha mara moja na endapo mwanafunzi au mtoto aonapo viashiria au afanyiwapo vitendo vya ukatili kama vipigo, ubakaji, ulawiti anatakiwa atoe taarifa kwa Jeshi la Polisi ili wahusika wachukuliwe

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.