RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameeleza matarajio
yake kwa Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii - TASAF katika kupambana na umasikini nchini.
Dk. Mwinyi ameyasema hayo, Ikulu,
Zanzibar alipozungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa wa Mfuko huo, Shedrack
Salmin Mziray aliefika
kujitambulisha kufuatia uteuzi wake hivi karibuni.
Alisema, anatarajia kupitia miradi ya
TASAF kwa kaya masikini nchini, itaendelea kuzisaidia kaya zilizo kwenye
mazingira magumu zaidi kwa lengo la kuwatoa kwenye umasikini mkubwa sambamba na
kutafuta mbinu mbadala kwa kaya zinazoendelea kuwa kwenye umasikini uliokithiri
licha ya kupitiwa na miradi ya TASAF.
Rais Dk Mwinyi pia ameupongeza uongozi wa
TASSAF kwa jitihada zao za kuinua ustawi wa jamii hasa kwa kuboresha maisha ya
familia 22,000 za Zanzibar kupitia mwondelezo wa miradi 15 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.1
vikiwemo vituo vya afya, madarasa, maji safi na salama pamoja na barabara za
vijijini.
Pia Rais Dk. Mwinyi alisema, miundombinu
hiyo imesaidia kukuza uchumi wa wananchi, kuwaongezea kipato, kwa kuzisaidia
kaya masikini kukuza mitaji yao ya biashara na kuwaongezea ajira ndogondogo.
Vilevile Rais Dk. Mwinyi alipongeza mpango
wa TASAF awamu ya pili kwa kuendeleza na kusaidia maeneo ambayo serikali zote
mbili bado hazijakamilisha.
Naye, Mkurugenzi Mziray alimueleza Rais Dk. Mwinyi kwamba kwasasa TASAF
inatekeleza kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya miradi yake tangu mwaka 2020
hadi kukamilika kwake mwezi Septemba mwaka 2025 ambapo TASAF inatekelezwa na Mamlaka
za utekelezaji 187, zikiwemo Halmashauri zote za Tanzania Bara, Unguja na
Pemba.
Alisema
TASAF inashughulika na asilimia 26 ya kaya masikini nchi nzima na asilimia nane
ni kaya masikini zaidi ziliwemo kaya milioni 1.3 wanazozipatia ruzuku kila
baada ya miezi miwili na ajira za muda kwa watu wenye uwezo wa kufanyakazi.
Mkurugenzi
huyo aliongeza kuwa wanazisaidia kaya hizo kuweka vikundi vya maendeleo kwa kuweka
na kuwekeza ili kuwaongezea mitaji kwa wastani wa shiingi laki tatu na nusu ili
wajiendeleze zaidi.
Alieleza
kwasasa TASAF inazishughulikia kaya 394,000 ambazo mradi umezifanyia tathmini
na zina mafanikio mkakubwa kati ya hizo kaya 22,000 kutoka Zanzibar ambapo kati
yao kaya18,000 zimenufaika na ruzuku za ziada za laki tatu tatu, wanaofanikiwa
wanatolewa kwenye mpango kupisha waliokua hawajafanikiwa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii – TASAF, bw. Shedrack Salmin Mziray
aliteuliwa kushika wadhifa alionao sasa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan Julai 03 mwaka huu, Kabla ya uteuzi wake bw.
Mziray alikuwa Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa TASAF, awali aliikaimu nafasi
hiyo ya Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF tokea Julai 01 mwaka 2023 baada ya
kustaafu kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji Bw. Ladislaus Joseph Mwamanga hadi
alipoteuliwa yeye mwezi mmoja uliopita.
IDARA YA MAWASILINO,
IKULU ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment