Dk. Mwinyi ameyasema hayo Ikulu, Zanzibar alizungumza
na Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dk. Ashatu Kijaji alieambatana na timu ya watendaji wakuu wa Wizara
hiyo, waliofika kwaajili ya kujitambulisha.
Amesema, ni vyema Wizara hizo mbili kuweka mkazo
katika kuzipitia Sera, kanuni miongozo,
mipango na mikakati ya kudhibiti changamoto za mazingira na mabadiliko ya
tabianchi kwa pamoja ili kubadilishana uzoefu na kuibua utatuzi wa masuala
hayo.
Amesema, uvamizi wa majichumvi kwenye maeneo ya
kilimo, visima na makaazi ya wananchi, mporomoko wa fukwe za bahari na ukosefu
wa mvua na mvua zisizotarajiwa bado ni matatizo yanayoathiri kwa kiasi kikubwa.
Rais Dk. Mwinyi amewataka watendaji wa wizara hizo
kutumia makongamano na mikutano ya kimataifa ya kimazingizingira kuziwasilisha
changamoto hizo zinaziikabili nchi ili kupata ufadhili na rasilimali za
kukabiliana nazo.
Aidha, aliwasisistiza kuwa na mipango shirikishi
kuanzia ngazi za chini kwa jamii ili nayo itoe mchango wake.
Pia, Dk. Mwinyi amesema, Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar imeendelea kuchukua juhudi mbalimbali za kuzuia athari za mazingira
zisiendelee kuathiri maisha ya watu.
Akizungumzia masuala ya Muungano, Rais Dk. Mwinyi
ameridhia ombi la Waziri Kijaji la kutaka siku tatu kila mwezi kwa watendaji wa
Wizara hizo mbili kukutana Zanzibar na kuwa na mikutano na wananchi kutoa maoni
yao juu ya changamoto za Muungano.
Kuhusu biashara ya kaboni, (gesi ukaa) Dk. Mwinyi
aliwataka watendaji hao kushirikiana kwa pamoja, kujengeana uwezo na kuwatafuta
wataalamu kwani biashara hiyo ni mpya ulimwenguni.
Pia, Dk. Mwinyi amesisitiza suala la Uratibu wa
shughuli za Muungano kwani sekta zote wanazozisimamia zinahitaji ushirikiano wa
karibu ili kuleta ufanisi.
Naye, Waziri Kijaji ameeleza tayari Wizara hiyo imeandaa
timu ya wataalamu na imeanza utafiti na kuandika miradi kwa lengo la
kuiwasilisha kwa wafadhili ili kupata fedha zitakazoendesha miradi ya
kimazingira.
Amebainisha, kuwa uharibifu wa mazingira ni mkubwa
hasa katika fukwe unaosababishwa na mmongonyoko na uvamizi wa maji chumvi
katika maene ya kilimo, hivyo juhudi za pamoja zinahitajika kukabiliana na hali
hiyo.
Waziri Kijaji amefika ikulu kujitambulisha baada ya
kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan,
Julai 03 mwaka huu.
IDARA YA
MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment