Habari za Punde

WAZIRI WA BIASHARA NA MAENDELEO YA VIWANDA AZUNGUMZA NA WAANDISHI ZANZIBAR

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said Shaabani akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Manesho ya Biashara ya Kimataifa ya Kumi na Moja (11)yatakayofanyika kuanzia Tarehe 1 January hadi Tarehe 15 kwa Unguja katika eneo la Nyamanzi na kwa Pemba yataanzia Tarehe 7 hadi 15 katika Eneo la Chamanangwe hafla iliofanyika katika Ofisi ya Wizara hio Kinazini Zanzibar.

Na Ali Issa Maelezo       4/12/2024

Wizara ya Biashara na Maendeleo ya  Viwanda Zanzibar itaendelea kufanya Maonyesho ya Biashara katika eneo lake la kudumu liliopo nyamazi kwa ajili ya maendeleo ya Nchii na wafanya Biashara wandani na nje ya Nchi.

 Waziri wa Wizara hiyo  Mhe Omar Said Shabani  huko Ofisini kwake  kwake kinazini mjini Unguja   wakati alipokuwa na mazunguzo na wandishi wa Habari.

Amesema kufuatia Sherehe za maadhimisho ya  Mapinduzi ya Zanzibar mwaka huu Zanzibar kila  Wizara huratibiwa kuwa na shughuli zake mbali mbali za miradi ya kimaendeleo 

Amesema kuwa kwa upande wao  mwaka  2025 licha ya kuwepo shughuli hizo za kimaendeleo pia wanatarajia kuwa na maeonyesho ya kibiashara ya Kimataifa  yatayo washirikisha wafanya Biashara mbalimbali  na wajasiriamali wandani na nje ya Nchi.

Alisema maeonyesho hayo yataaza Junari mosi hadi Januari 15 kwa Unguja na yatashirikisha wafanyabishara na wajasiriamali 500 kwa Unguja na kwa Upande  Pemba yanatarajiwa kuaza Januari saba(7)  hadi15 katika viwanja vya Chamanangwe na yatashirikisha wafanya Biashara na wajasiriamali 100 na kuwataka wafanya bishara  kwenda  kujisajili.

Alifahamisha kuwa maeonyesho hayo ni upatikanaji  frusa za masoko kwa wafanya Biashara kwani watapata nafasi ya kuuza bidhaa zao na kuzitangaza kitaifa na kimataifa.

Pamoja na hayo alisema kuwa wanadhamira ya kuwapatia semina wafanya Biashara ili kufanya biashara zao zaidi kimtandao na kidijitali njia ya kisasa ya kuuza bidhaa kidijitali na kuzitangaza katika masoko duniani.

Aidha alisema mwaka huu wametoa ofa maalum ya punguzo la asilimia kumi (10) kwa Jumuiya ya  wafanyabishara wanawake ambao wamejisajili na wamesajiliwa na Jumuiya hiyo ikiwa ni kuwapa hamasa zaidi kufanya biashara.

Maeonyesho hayo ya 11 ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu Biashara mtandao kwa maendeleo ya Biashara na uwekezaji.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika mkutano wa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said Shaabani  akizungumza  kuhusiana na Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Kumi na Moja (11)yatakayofanyika kuanzia Tarehe 1 January hadi Tarehe 15 kwa Unguja katika eneo la Nyamanzi na kwa Pemba yataanzia Tarehe 7 hadi 15 katika Eneo la Chamanangwe hafla iliofanyika katika Ofisi ya Wizara hio Kinazini Zanzibar.
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said Shaabani (Kushoto)akimsikiliza Mwandishi wa Habari wa ITV Farouk Karim akiuliza maswali katika mkutano wa Waziri na Waandishi wa Habari akizungumza  kuhusiana na Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Kumi na Moja (11)yatakayofanyika kuanzia Tarehe 1 January hadi Tarehe 15 kwa Unguja katika eneo la Nyamanzi na kwa Pemba yataanzia Tarehe 7 hadi 15 katika Eneo la Chamanangwe hafla iliofanyika katika Ofisi ya Wizara hio Kinazini Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika mkutano wa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said Shaabani  akizungumza  kuhusiana na Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Kumi na Moja (11)yatakayofanyika kuanzia Tarehe 1 January hadi Tarehe 15 kwa Unguja katika eneo la Nyamanzi na kwa Pemba yataanzia Tarehe 7 hadi 15 katika Eneo la Chamanangwe hafla iliofanyika katika Ofisi ya Wizara hio Kinazini Zanzibar.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.